Kamwe Usipoteze Matumaini Katika Kumrekebisha Mtu Yoyote

Kamwe Usipoteze Matumaini Katika Kumrekebisha Mtu Yoyote

Abdullah bin Maslamah Qa’nabi (rahimahullah) alikuwa miongoni mwa Muhadditheen mashuhuri katika zama zake. Alikuwa ni ustaad wa Muhadditheen wengi mashuhuri, kama Imaam Bukhaari, Imaam Muslim na Imaam Abu Daawuud (Rahimahumullah).

Inaripotiwa kwamba mwanzoni mwa maisha yake, alikuwa na marafiki wabaya na alikuwa akinywa pombe.

Hata hivyo, baada ya kukutana na Muhaddith mkubwa na mtakatifu, Imaam Shu’bah (rahimahullah), kulikuwa na mabadiliko kamili ambayo yaliingia katika maisha yake na akawa miongoni mwa vinara wa Uislamu.

Ifuatayo ni tukio ambalo lilimpelekea kutubu na kurekebishwa:

Wakati fulani Abdullah bin Maslamah alikaa mbele ya mlango wa nyumbani kwake akisubiri marafiki zake wafike. Akiwa ameketi, alimuona Muhaddith mkubwa, Imaam Shu’bah (rahimahullah), akipita karibu na nyumba yake, amepanda punda wake.

Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakitembea kando na nyuma ya punda wa Imaam Shu’bah (rahimahullah), kwa nia ya kunufaika na maneno yake na kundi lake.

Alipomtazama Imaam Shu’bah (rahimahullah) na umati mkubwa wa watu waliomzunguka, Abdullah bin Maslamah alimuuliza mtu mmoja aliyekuwepo, “Mtu huyu ni nani?” Yule mtu akajibu, “huyu ni Imaam Shu’bah (rahimahullah).”

Abdullah bin Maslamah akauliza, “Kazi yake ni nini?” mtu huyo akajibu, “Yeye ni Muhadith (mtu anayesimulia hadith za Mtume Sallallahu alaihi wasallam).

Kusikia hivyo, Abdullah bin Maslamah, aliyekuwa amevaa kikoyi chekundu wakati huo, alisimama na kusogea kukutana na Imaam Shu’bah (rahimahullah). Alipomfikia Imaam Shu’bah (rahimahullah), alizungumza naye kwa njia ya ukusowefu wa adabu akimwambia, “Nisimulie Hadith.”

Akitazama sura ya nje ya Abdullah bin Maslamah, Imaam Shu’bah (rahimahullah) aligundua kwamba mtu huyu alikuwa ni mtu asiyekuwa imara kwenye dini.

Kwa hiyo, Imaam Shu’bah akajibu: “Vipi nikuhadithie hadithi na hali wewe si miongoni mwa wanafunzi wa Hadith! (hujavaa vizuri na hauna adabu ya wale ambao wanataka kusoma hadith za mtume Sallallahu alaihi wasallam).

Abdullah bin Maslamah aliposikia hivyo alikasirika. Alichomoa kisu chake na kumtishia Imaam Shu’bah (rahimahullah) kwa kusema, “Ama unisimulie Hadith sasa au nitakuchoma!”

Imaam Shu’bah (rahimahullah) hivyo alianza kusimulia, “Mansoor anaripoti kutoka kwa Rib’ee, ambaye anasimulia kutoka kwa Abu Mas’uud kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, ‘Ikiwa hauna sifa ya hayaa (aibu), basi fanya upendavyo (yaani pale mtu anapokuwa hana hayaa, basi hatokuwa na heshima ndani yake na atakuwa tayari kufanya dhambi ya aina yoyote).”

Imaam Shu’bah (rahimahullah) alikuwa ni mtu wa kufuata Sunnah ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Ndo maana pindi haya maneno yaliingia moyoni mwake, yalikuwa na athari kubwa moyoni mwa Abdullah bin Maslamah hadi akawa anajuta na akatubu kwa ikhlaas madhambi zake.

Akatupa kisu chake chini, akarudi nyumbani na kumwaga pombe zake zote.

Baada ya hapo akamwambia mama yake: “Rafiki zangu watakuja hivi karibuni. Wakija basi waruhusu waingie na uwakirimu chakula, wakisha kula, basi wajulishe kwamba nimebadili maisha yangu na nimemwaga pombe zangu zote.

Kisha akaondoka kuelekea Madinah Munawwarah kwa nia ya kubadilisha maisha yake na kusoma Hadith chini ya Imaam mkubwa wa wakati, Imaam Maalik (rahimahullah).

Akabaki na Imaam Maalik (rahimahullah) mpaka Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) Akambariki na mali ya Dini na akawa Imaam mkubwa katika elimu ya Hadith.

Kutokana na tukio hili, tunaelewa kwamba mtu hapaswi kamwe kupoteza matumaini ya kumrekebisha mtu yeyote.

Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiishi maisha ya kumuaasi Allah, lakini wakarejea kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) ya ikhlaas. Kisha wakajiunganisha na marafiki maalum wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala), na wakarekebisha maisha yao kwa kubaki pamoja nao.

Baada ya hapo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) Akawabariki kwa uchamungu na ukubalifu kiasi kwamba wakawa vielelezo kwa umma kufuata.

About admin

Check Also

Kuwa Na Moyo Wa Kusamehe

Waa’il bin Hujr (Radhiyallahu anhu) alikuwa sahaabi maarufu wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ambaye alitoka …