
Wakati wa vita vya Hunain, Waislamu walipata kushindwa kwa muda. Katika kipindi hiki kigumu, Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliobaki imara na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).
Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia:
“Nilikuwa pamoja na Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) siku ya Hunain wakati Waislamu walipoanza kukimbia kutoka kwenye uwanja wa vita. Hata hivyo watu thamanini kutoka wa muhajireen na Answaar walikuwa imara pamoja na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).
Tulirudi nyuma kidogo kwa takriban futi themanini, lakini hatukugeuza migongo yetu kwa adui na kukimbia (uwanja wa vita). Hawa ndio Waumini ambao Mwenyezi Mungu aliwateremshia Sakinah (utulivu katika uwanja wa vita).
Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaendelea kusimulia kwamba: “Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa amekaa juu ya punda wake, alikuwa akimsukuma punda wake kusonga mbele kumuelekea adui. Punda wake alihangaika na kuyumba kuelekea upande mwingine, na kusababisha Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kusogea kidogo upande mmoja wa tandiko. Nilikuwa na wasiwasi juu ya Rasululah (Sallallahu alaihi wasallam) kudondoka kutoka kwa mnyama na hivyo nikamwambia, ‘(Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Sallallahu alaihi wasallam)), simama imara (kwenye tandiko). Allah Ta’ala akupandishe juu!’
Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akaniambia, ‘Nipe mchanga kiasi ya kujaa mkono.’ Kisha akautupa (mchanga) kwenye nyuso zao (nyuso za madui), na kupitia mchanga huo, Allah Ta’ala akayafanya macho ya madui kujaa na mchanga huo.
Baada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akauliza: ‘Wako wapi Muhajirina na Answaar?’ Nikajibu: ‘Wapo pale (kwenye uwanja wa vita).’ Kisha akasema: ‘Waiteni.
Basi nikawaita, nao wakaja mbele wakiwa wamebeba mipanga zao, zikimulika kama nyota kwenye mikono yao ya kulia. Kwa kuona haya, waMushrikeen waligeuza migongo yao na wakakimbia (uwanja wa vita). Kwa njia hii, Mwenyezi Mungu alimbariki Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na Maswahabah kwa ushindi.” (Musnad Ahmad #4336)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu