Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا مجالسكم بالصلاة علي فإن صلاتكم علي نور لكم يوم القيامة (الفردوس بمأثور الخطاب، الرقم: ٣٣٣٠، وإسناده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٨)

Ibnu umar (radhiyallahu anhuma) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alisema, “Pamba mikusanyiko yenu na kunitumia salaam, kwa sababu siku ya qiyaama, salamu zenu juu yangu itakuwa nuru (sababu ya nuru) kwenu.”

Kubaki katika kundi la wale wanaomswalia Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam)

Sa’d Zanjaani (rahimahullah) aliwahi kuhadisia yafuatayo:

Kulikuwa mchamungu ambae alikuwa anaishi Egypt. Alikuwa anaitwa Abu Sa’eed Al-Khayyaat (rahimahullah) Alikuwa hachanganyi na kushirikiana na watu, wala alikuwa ashiriki kwenye vikao vyovyote vile. Ila, baada ya muda kadha, akaanza kushiriki kikao cha Ibnu Rasheeq
(rahimahullah).

Pindi watu waligundua hili, walishtuka na wakamuuliza sababu ya kushiriki kikao cha Ibnu Rasheeq (rahimahullah). Abu Sa’eed Al-Khayyaat (rahimahullah) akajibu, “nilimuona Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Kwenye ndoto na akaniambia, ‘hudhuria kikao cha Ibnu Rasheeq (rahimahullah), kwa sababu ananitumiaga salaam kwa wingi juu yangu.” (Al-Qawlul Badee, Pg, 131)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …