Kupata Maombezi Ya Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

عن رويفع بن ثابت قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى على محمد وقال: اللهم أنزله المقعد المقرب عندك يوم القيامة، وجبت له شفاعتي (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: ٤٤٨٠، وإسناده حسن كما في مجمع الزوائد، الرقم: ١٧٣٠٤)

Sayyidina Ruwaifi Bin Thaabit Al ansaari (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “yoyote atakae soma dua hii ifuatayo, msaada wangu utakuwa wajibu juu yake siku ya qiyama

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ وَأَنْزِلْهُ الْمَقْعَدَ الْمُقَرَّبَ عِنْدَكَ يَوْمَ الْقِيَامَة

Ewe  Allah subhaana wata’alah! Tuma salaam kwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na umjalie nafasi ya ukaribu kwako siku ya mwisho.

Maelezo: kulingana na baadhi ya muhadditheen, “nafasi ya ukaribu” imetajwa ndani ya hadith kuhusu utukufu wa kuombewa kwa niyaba ya umma mzima ili hesabu iyanze siku ya qiyama (maqaam e mahmood). Kulingana na muhaddith wengine inahusu nafasi inayoheshimika sana na iliyoinuliwa uko jannah, kulingana na hali ya Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Jiwe Lilokuwa Linatowa Salaamu Kwa Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Sayyidina Jaabir Bin Samurah (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “hakika kuna jiwe ninalifahamu  makkah lilikuwa linanitolea salaam kabla yangu ya kupokea utume hakika ninalitambuwa hilo jiwe hadi sasa.” (Musnad Ahmed #17565)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …