Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Akimuobea Msamaha Mtu

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: أكثروا الصلاة علي في الليلة الزهراء واليوم الأزهر فإن صلاتكم تعرض علي فأدعو لكم وأستغفر (القربة لابن بشكوال، الرقم: ١٠٧، وسنده ضعيف كما في المقاصد الحسنة، الرقم: ١٤٨)

Sayyidina Umar Bin Khattaab (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “zidisheni kunitumia mimi salaam usiku wa ijumaa na mchana wa ijumaa kwa sababu salaam zenu zinaletwa kwangu. Kisha naomba dua kwa ajili yako na muomba Allah subhaana wata’alah akusamehe madhambi yako.”

Mti Ambao Ulimsalimia Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Sayyidina Ya’laa Bin Murrah Thaqafee (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti:

Wakati mmoja tulisafari na Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pindi tumekaa sehemu fulani. Baada ya kukaa, Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alienda kulala. Baada ya hapo, mti ukaja, kwa kutengeneza njia yake kwenye ardhi, mpaka ukampa kivuli Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam), baada ya hapo ukaacha na kurudi sehemu yake.

Pindi Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipo amka, nilimuhadithia kilichotokea. Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “ulikuwa ni mti ambao umemuomba mola wake rukhusa (kuja kwangu na) kutoa salaam kwangu. Allah subhaana wata’alah aliupa rukhusa huo mti. (Musnad Ahmed, #17565)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …