Kutokomeza Kwa Umasikini

وعن سمرة السوائي والد جابر رضي الله عنهما قال: كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم  إذ جاءه رجل فقال يا رسول الله ما أقرب الاعمال الى الله قال صدق الحديث وأداء الامانة، قلت يا رسول الله زدنا قال صلاة الليل وصوم الهواجر قلت يا رسول الله زدنا قال كثرة الذكر والصلاة علي  تنفي الفقر قلت يا رسول الله زدنا قال من أم قوما فليخفف فإن فيهم الكبير والعليل والصغير وذا الحاجة (معرفة الصحابة لأبي نعيم، الرقم:  ٣٥٧٢ ،وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ ٢٧٨)

Sayyidina Samurah Suwaai (radhiallahu anhu), baba wa Sayyidina Jaabir (radhiallahu anhu), ameripoti kwamba: tuliwahi kuwa na Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) pindi mtu mmoja alikuja kwa Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na akauliza, ” ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) !ni tendo gani linalomrizisha Allah subhaana wata’alah zaidi?” Nabii wa Allah-(sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “maneno ya ukweli na kutimiza uwaminifu.” Nikasema, “ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha (kuhusu matendo yanayo mrizisha Allah subhaana wata’alah)!” Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, ” swali wakati wa usiku na funga wakati wa jua kali.” Kisha nikasema, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Nakuomba utuzidishie nasaha!” Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, ” jishughulishe na zikr kwa wingi na nitumie salaam inaondowa umasikini,” nikauliza tena, ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) nakuomba utuzidishie nasaha! Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) akasema, yule atakae  swalisha  watu basi  afupishe swala,kwa sababu kwenye jamaa  kuna wazee, kuna wagonjwa, vijana na watu kuna ambao wana dharura.”

Mapenzi Ya Nabii Wa Alllah Kwa Ummah Wake

Imerikodiwa ndani ya “Mawaahib Ladunniyah” kutoka kwenye ” tafseer qushairy” kwamba siku ya qiyama, muumini atatokea kwa hesabu na mzaani mdogo wa matendo yake mazuri. Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) atatokea, na ataweka kwa upande wa mazuri yake, karatasi ndogo usawa wake ni kama ncha ya kidole. Matokeo yatakuwa kwamba mzaani wa matendo mazuri yanazidi mzaani wa matendo mabaya na mbali.

Kuona hili, muumini atashangaa na kusema, wazazi wangu wajitolea kwa ajili yako, wewe ni nani? Vipi muonekano wako wa mwili ni mzuri, na mwenendo wako ni mtukufu kiasi gani !” Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) Alijibu, ” hakika mimi ni Nabii wako (sallallahu alaihi wasallam). Hii niliyoweka kwenye mzaani wako ni salaam na swala ambazo ulikuwa unanitumia wakati wa uhai wako. Leo nimekuja kukusaidia kwenye muda wako wa shida.”  (Sharhuz Zurqani allal Mawahib 359/12)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …