
‘Allaamah Zurqaani (Rahimahullah) amenukuu tukio lifuatalo Kutoka kwa Haafidh Ibn ‘Asaakir (Rahimahullah) na sanad ya nguvu ya wasimulizi:
Baada ya Rasulullah (Sallallahu Alaihi Wasaalm) kufariki, ilikuwa ngumu kwa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kuendelea kuishi Madinah Munawwarah kutokana na upendo wake mkubwa kwa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi wasallam) katika mji uliobarikiwa.
Kwa hivyo, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) aliondoka Madinah Munawwarah na kuishi katika Daariyyaa (mahali palipo Syria). Baada ya muda, wakati akiishi Syria, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) Usiku mmoja alimuona Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) katika ndoto. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alimwambia akisema, “Ewe Bilaal! Kwanini umejitenga na mimi? Sio wakati wa wewe kuja kunitembelea?”
Wakati Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alipoamka usingizini, alijazwa na huzuni na wasiwasi hadi mara moja akaanza safari yake na kweda Madinah Munawwarah.
Alipofika mbele ya kaburi lililobarikiwa la Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam), alishindwa kuvumila kwa ajili ya upendo wa kina kwa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) na huzuni mkubwa kwa kujitenga kwake hadi akaanza kulia.
Hasan na Husain (Radhiyallahu ‘Anhuma) baadaye walikutana naye. Alipowaona, Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) alimkumbatia na kumbusu kwa upendo aliokuwa nao kwa familia ya Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam). Baadaye walimwambia Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu), “Tunatamani kusikia ukitoa Adhaan kama jinsi ulikuwa ukitoa kwa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam).”
Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kwa hivyo alipanda mahali pa kuinuliwa ili atoe Adhaan. Alipoanza kutoa Adhaan akisema “Allahu Akbar Allahu Akbar!” Mitaa ya Madinah Munawwarah ulianza kusikika na sauti yake.
Alipoendelea na kusema maneno yafuatayo ya Adhaan, sauti yake huko Madinah Munawwarah iliongezeka, na kuwafikia watu, hadi wanawake na watoto walitoka majumbani kwao. Wote walionekana wakilia nje kwa kukumbuka enzi ya Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam). Huo ndio ulikuwa upendo wa hali ya juu waliyokuwa nayo kwa Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) ambayo hapokuwa na siku baada ya kufariki kwa Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) ambayo watu wa Madinah Munawwarah walilia zaidi kuliko siku hiyo.
(Zurqaani 5/71)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu