Fadhila Za Kusoma Quran Takatifu 2

Allah Ta’ala Anamsikiliza Mwenye Kusoma kwa Furaha Nyingi

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) hasikilizi chochote (kwa furaha nyingi) kama vile Akimsikiliza Nabii yoyote kwa sauti nzuri yenye kupendeza akisoma Qur’an Takatifu kwa sauti.”[1]

Dua Zikijibiwa Katika Kuhitimu Quran

Irbaadh bin Saariyah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Nabi wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mwenye kuswali swalah yake ya fardh (kwa utaratibu sahihi), basi kwake kuna dua ambayo hakika itajibiwa. Mwenye kuhitimu Qur-aan Takatifu, basi kwake kuna dua itakayojibiwa.”[2]

Malaika Wakimuombea Msamaha kwa Mwenye kuhitimu Qur’aan

Sa’d bin Abi Waqqaas (radhiyallahu ‘anhu) alisema, “Wakati mtu akihitimu Qur’an Takatifu jioni, Malaika wanamuombea msamaha mpaka asubuhi, na anapo hitimu Quran Takatifu asubuhi, Malaika humtakia maghfirah mpaka jioni”.[3]

Kitendo Ambacho Ni Kipenzi Zaidi kwa Allah Ta’ala – Kuendelea Kusoma Quran Takatifu Mara Kwa Mara

Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba mtu mmoja alimuuliza Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam): “Ni kitendo gani kinachopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)? Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, ‘Kitendo cha haal na murtahil (msafiri ambaye baada ya kumaliza safari yake, anaanza upya tena safari yake)’. Yule mtu akauliza, ‘Ewe Rasullulah (sallallahu ‘alaihi wasallam), kwa kusema kitendo cha haal na murtahil (msafiri ambaye baada ya kumaliza safari yake anaanza upya tena safari yake), unammaanisha nani?’ Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, “Ninamzungumzia msomaji wa Quraan Takatifu ambaye (wakati wa safari yake ya kusoma Kitabu cha Allah Ta’ala) anasoma kuanzia mwanzo wa Quraan Takatifu mpaka mwisho, na atakapofika mwisho (wa Qur-aan Takatifu ), basi anaanza tena upya (Qur’an Takatifu toka mwanzo).[4]


[1] صحيح البخاري، الرقم: 7544

[2] المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 647، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله مجمع الزوائد، الرقم: 11712: رواه الطبراني، وفيه عبد الحميد بن سليمان وهو ضعيف

[3] سنن الدارمي، الرقم: 3526 وقال: هذا حسن عن سعد

[4] سنن الترمذي، الرقم: 2948، وقال: هذا حديث غريب لا نعرفه من حديث ابن عباس إلا من هذا الوجه وإسناده ليس بالقوي، وقال الحاكم: له شاهد من حديث أبي هريرة، عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قام رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله أي العمل أفضل أو أي العمل أحب إلى الله قال: الحال المرتحل الذي يفتح القرآن ويختمه صاحب القرآن يضرب من أوله إلى آخره ومن آخره إلى أوله كلما حل ارتحل (المستدرك على الصحيحين للحاكم، الرقم: 2090)

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …