Umar (radhiya alaahu ‘anhu) Akiwaheshimu Azwaaj-ul-Mutahharaat (radhiyallahu ‘anhun)

Aslam (rahimahullah), mtumwa wa Umar (radhiyallahu ‘anhu), anaripoti kwamba Umar (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa na sahani tisa maalum zilizohifadhiwa kwa ajili ya kutuma zawadi kwa Azwaaj-ul-Mutahharaat (wakezake na Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na mama wa ummah.

Aslam (rahimahullah) alitaja kwamba wakati wowote chakula kizuri, tunda au nyama inapomjia Umar (radhiya allaahu ‘anhu), basi alikuwa akifanya hisa tisa, aziweke kwenye sahani tisa na kuzipeleka kwa Azwaaj-ul-Mutahharaat kwa heshima.

Alikuwa akipeleka sahani nane za kwanza kwa Azwaj-e-Mutahharaat na akituma sinia ya mwisho kwa binti yake mpendwa, Hafsah (radhiyallahu ‘anha).

Kuna wakati ikitokea kuwa na upungufu kidogo katika sinia yoyote, basi alikuwa akituma sahani hio kwa binti yake kipenzi, Hafsah (radhiyallahu ‘anha), na kuhakikisha kwamba wake wengine wa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) wanapokea sinia kamili. Kwa njia hii, Umar (radhiya allaahu ‘anhu) alitoa upendeleo kwa wake wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuliko familia yake mwenyewe. (Muwatta Imaam Muhammad #405)

About admin

Check Also

Ukarimu Wa Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiyallahu ‘Anhu)

Miswar bin Makhramah (Radhiya Allaahu anhu) anaripoti: Abdur Rahmaan bin Auf (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakati …