1. Elekea kibla.
2. Weka miguu pamoja au karibu iwezekanavyo. Hakikisha kwamba miguu inaelekea kibla.
3. Baada ya hapo, weka nia ya Swalaah unayoswali na inua mikono yako mpaka vidole gumba viwe sawa sawa na ncha za masikio na ncha za vidole vyako viwe sawa sawa na sehemu ya juu ya masikio yako.
4. Wakati wa kuinua mikono mpaka kufika kwenye masikio, hakikisha kwamba viganja vya mkono vinaelekea kibla na vidole vipo mbali kidogo bila kugusana.
5. Anza takbira pindi unapo inua mikono yako na malizia takbira pindi unapokunja mikono.
6. Wakati wa kusoma takbeera tul ihram (takbira ya kwanza), hakikisha kwamba macho yako yanaangalia sehemu ya kusujudu na kichwa chako kimeteremshwa kidogo.
7. Ikunje mikono chini ya kifua na juu ya kitovu.
8. Shika kifundo cha mkono wa kushoto na mkono wa kulia na pia weka vidole vya mkono wa kulia kwenye kiganja cha mkono wa kushoto.
9. Weka macho kwenye sehemu ya kusujudu wakati unaposimama.