Wakati wa kutoa adhaan, mtu ajitahidi kutamka maneno kwa usahihi. Katika suala hili, baadhi ya nukta muhimu kuzikumbuka ni:
1. Wakati wa kusema اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ ,herufu ر (Raa) katika أَكْبَرْ (Akbar) ya kwanza itasemwa na fat-hah (ــَـ) (kwa kuiunganisha na neno اللهُ (Allahu).
2. Pindi unapo sema أَشْهَدُ أَلَّا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ, Neno أَلَّا (Al-laa) inabidi isomwe na mdomo wazi. Vile vile tashdeed (ــّـ) yenyewe ipo juu ya ل (Laam) inabidi isemwe Kwa msisitizo Kwa kukaza sauti ya ل (Laam).
Sukoon (ــْـ) au sakna juu ya ش (Sheen) isomwe vizuri na kuonganishwa na هـ (Haa). Sakna kwenye ش (Sheen) na herufu هـ (Haa) isiachane Kwa kuunganisha herufu هـ (Haa) kwenye ش (Sheen) na kusema “ashadu” bila kutaamka herufu هـ (Haa) kabisa. Kwa hiyo njia sahihi kutamka ni “ash – ha – du”.
3. Pindi unapo sema أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَّسُوْلُ اللهْ , Neno أَنَّ (Anna) haitakiwi kuvuta sana tashdeed kwenye ن (Noon) zaidi ya muda wa kusoma ghunnah. Vile vile tashdeed (ــّـ) Kwenye herufu م (Meem) na ر (Raa) haitakiwi pia kuvutwa sana.
4. Pindi unaposema حَيَّ عَلٰى الصَّلَاةْ, Tashdeed (ــّـ) Kwenye herufu ي (Yaa) kwenye neno حَيَّ (Hayya) inatakiwa kusomwa kwa ukamilifu. Ile ي (Yaa) haitakiwi kusomwa bila tashdeed (ــّـ) Kwa kusema “haya” badala ya “hayya”. Vili vile herufu ع (‘ain) kwenye neno على (‘ala) inabidi isemwe vizuri.
Pindi unapoishia mwisho wa neno الصَّلَاةْ (Swalaah), ile ة (Taa) itasemwa na sakna (ــْـ) Na kuwa na sauti ya هـ ( Haa). Haitakiwi mtu kusoma ile ة (Taa) Kwa kusema “hayya ‘alas swalaaht.
Vile vile inabidi kuakikisha Kwamba sauti ya ة (Taa) isifanane na sauti ya herufu ح (Haa).
5. Pindi unaposema حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ , Wakati unapoishia kwenye neno الْفَلَاحْ (Falaah), hakikisha herufu ح (Haa) inasomwa Kwa usahihi Kwa kuisoma Kama ح (Haa) na sio هـ.