Maneno ya Iqaamah na Njia ya Sunnah ya kutoa Iqaamah

1. Maneno ya iqaamah ni sawa sawa na maneno ya adhaan. Kwa hivyo, wakati wa kutoa iqaamah, inapaswa kusomwa kila kifungu cha maneno mara moja, isipokuwa قَدْ قَامَتِ الصَّلاَةْ (Qad Qaamatis Swalaah) ambayo itasemwa mara mbili. Kwa hivyo, baada ya حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ (hayya ‘alal falaah), mtu atasema:

قَدْ قَامَتِ الصَّلَاةْ قَدْ قَامَتِ الصَّلَاةْ

Swalaah imethibiti, Swalaah imethibiti.[1]

2. Wakati wa kutoa iqaamah, soma maneno mawili kwa pamoja na sitisha tu baada ya kukamilisha vishazi vyote viwili. Namna ya kusoma kila seti ya vishazi viwili ni kama ifuatavyo:[2]

Kwanza sema:

اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ

Allah ta’ala ndiye mkubwa , Allah ta’ala ndiye mkubwa.

Pili sema:

أَشْهَدُ أَلَّا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَّسُوْلُ اللهْ

Na Shuhudia kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Allah ta’ala. Nashuhudia kwamba Sayyiduna Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) ni mjumbe wa Allah ta’ala

Tatu sema:

حَيَّ عَلٰى الصَّلَاةْ حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ

Njooni kwenye Swalaah, njooni kwenye mafanikio.

Nne sema:

حَيَّ عَلٰى الصَّلَاةْ حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ

Swalaah imethibiti, Swalaah imethibiti.

Tano sema:

اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ

Allah ta’ala ndiye mkubwa, Allah ta’ala ndiye mkubwa.

Sita sema:

لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ

Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ta’ala

Maelezo: ة (taa) ya neno الصَّلَاةْ (swalaah) katika حَيَّ عَلٰى الصَّلاَهْ (hayya ‘alal swalaah) na katika قَدْ قَامَتِ الصَّلاَهْ (qad qaamatis swalaah) inatakiwa isomwe na sukoon (ــْـ) na kuisoma kwa kutoa sauti ya هـ (haa). Mtu hatakiwi kutatamka ة (taa) katika zote mbili. Vile vile, wakati wa kusoma misemo yote miwili katika iqaamah, mtu hatakiwi kusema hayya ‘alas swalaa ti hayya ‘alal falaah na qad qaamatis swalaa tu qad qaamatis salaat. Badala yake, mtu atasema hayya ‘alas swalaah hayya alah falaah na qad qaamatis swalaah qad qaamatis swalah.


[1] والاقامة إحدى عشرة كلمة الله أكبر الله أكبر أشهد أن لا إله إلا الله أشهد أن محمدا رسول الله حي على الصلاة حي على الفلاح قد قامت الصلاة قد قامت الصلاة الله أكبر الله أكبر لا إله إلا الله … وأما الإقامة ففيها خمسة أقوال الصحيح أنها إحدى عشرة كلمة كما ذكره المصنف وهذا هو القول الجديد وقطع به كثيرون من الأصحاب (المجموع شرح المهذب 3/69-71)

[2] وفي الإقامة يجمع كل كلمتين بصوت (المجموع شرح المهذب 3/95)

وكلمات الإقامة مشهورة وعدتها إحدى عشرة كلمة (ويسن إدراجها) أي الإسراع بها مع بيان حروفها فيجمع بين كل كلمتين منها بصوت والكلمة الأخيرة بصوت (مغني المحتاج 1/327)

يستحب ترتيل الأذان وإدراج الإقامة فالترتيل تبيين كلماته بلا بطء يجاوز الحد والإدراج أن يحدرها بلا فصل (روضة الطالبين 1/310)

قال المصنف رحمه الله (والمستحب أن يترسل في الاذان ويدرج الاقامة) … هذا الحكم الذي ذكره متفق عليه وهكذا نص عليه الشافعي في الأم (المجموع شرح المهذب 3/82)

About admin

Check Also

Dua wakati wa Adhaan ya Maghrib

Soma dua ifuatayo wakati wa adhaan ya Maghrib au baada ya adhaan:[1] اَللّٰهُمَّ إِنَّ هٰذَا …