Miaka Thamanini ya Kusamehewa madhambi, na Miaka Thamanini ya Ibaadah Inarikodiwa kwa kumswalia Nabii wa Allah Mara Thamanini kwenye siku ya Ijumaa

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى صلاة العصر من يوم الجمعة فقال قبل أن يقوم من مكانه اللهم صل على محمد النبي الأمي وعلى آله وسلم تسليما غفرت له ذنوب ثمانين عاما وكتبت له عبادة ثمانين سنة (القول البديع صـ 399)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kuswali Swalah ya Al-Asiri siku ya Ijumaa na kisha akatuma salaa na salaam ifuatayo mara thamanini kabla ya kusimama kutoka mahali pake, atasamehewa miaka thamanini ya madhambi na miaka thamanini ya ibaadah (nafl) atandikiwa:

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ وَعَلٰى آلِهِ وَسَلِّمْ تَسْلِيْمًا

Ewe Allah, tuma salaa na salaam tele juu ya Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) Nabii asiye jua kusoma, na juu ya familia yake.

Maisha na Mali ya Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) Kutolewa kafara kwa ajili ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Hadhrat Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba wakati mmoja Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Hakuna mali ya mtu iliyoninufaisha mimi kama mali na utajiri wa Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) Aliposikia haya, Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) akalia sana na akasema, “Ewe Mtume wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) hakika maisha yangu yote na mali zangu yote ni zako.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …