اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾ كَلّا إِنَّ الإِنسانَ لَيَطغىٰ ﴿٦﴾ أَن رَاهُ استَغنىٰ ﴿٧﴾ إِنَّ إِلىٰ رَبِّكَ الرُّجعىٰ ﴿٨﴾ أَرَءَيتَ الَّذى يَنهىٰ ﴿٩﴾ عَبدًا إِذا صَلّىٰ ﴿١٠﴾ أَرَءَيتَ إِن كانَ عَلَى الهُدىٰ ﴿١١﴾ أَو أَمَرَ بِالتَّقوىٰ ﴿١٢﴾ أَرَءَيتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلّىٰ ﴿١٣﴾ أَلَم يَعلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرىٰ ﴿١٤﴾ كَلّا لَئِن لَم يَنتَهِ لَنَسفَعًا بِالنّاصِيَةِ ﴿١٥﴾ ناصِيَةٍ كـٰذِبَةٍ خاطِئَةٍ ﴿١٦﴾ فَليَدعُ نادِيَهُ ﴿١٧﴾ سَنَدعُ الزَّبانِيَةَ ﴿١٨﴾ كَلّا لا تُطِعهُ وَاسجُد وَاقتَرِب ﴿١٩﴾
Soma kwa jina la mola wako ambaye ameumba (kila kitu). Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, na mola wako ni Mwingi wa Rehema. Ambaye amemfundisha (mwanadamu) kwa njia ya kalamu. Alimfundisha mwanadamu asiyoyajua. Kwa hakika, mwanadamu amekiuka mipaka yote, kwa sababu anajiona kuwa yuko huru. Hakika marejeo ni kwa Mola wako. Je, umemuona (Abu Jahl) ambaye anamsmamisha, mja (Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)) anaposimama katika Swalaah? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (mja – Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)) yuko juu ya uongofu, au anaamrisha kwa uchamungu (basi vipi Abu Jahl atamzuia)? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (Abu Jahl) atakataa na akageuka – hatambui kwamba Allah Ta’ala anaona kila kitu? Bali ikiwa (Abu Jahl) hataacha (maovu yake), tutamburuta kwa kisogo, kisogo cha uwongo mpotovu. Basi na aliite baraza lake, nasi tutaliita jeshi letu maalumu (la Malaika). Hapana! .Usimtii yeye (Ewe Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)), na uwe una sujudu na ukaribie (kwa Allah Ta’ala).
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾ كَلّا إِنَّ الإِنسانَ لَيَطغىٰ
Soma kwa jina la mola wako ambaye ameumba (kila kitu). Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, na mola wako ni Mwingi wa Rehema. Ambaye amemfundisha (mwanadamu) kwa njia ya kalamu. Alimfundisha mwanadamu asiyoyajua.
Kutoka katika Qur-aan tukufu yote, aya hizi tano zilikuwa Ayah za mwanzo kuteremshwa. Mwanzo wa wahi (wahyi) ulianza kwa Rasulullah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuonyeshwa katika ndoto za kweli. Chochote alichokuwa akikiona katika ndoto yake usiku, alikuwa akiona kikitokea katika uhalisia na kutokea mbele ya macho yake kwa uwazi kama mwanga wa alfajiri.
Baada ya hapo, alipata raha ya kujitenga katika pango la Hira kwenye Jabal Al Noor. Alikuwa akichukua chakula pamoja naye na kubaki katika upweke ndani ya pango, akijishughulisha na kumkumbuka Allah Ta’ala kwa muda mrefu. Kuna wakati fulani, alikuwa akishughulika na ukumbusho wa Allah Ta’ala ndani ya pango kwa muda wa siku kumi, na wakati fulani kwa siku ishirini, na wakati fulani, muda huo ungeendelea hata mwezi mmoja.
Kuna wakati mmoja, alikuwa akijitenga ndani ya pango, Jibraeel (‘alayhis salaam) alitokea mbele yake na kusema, “Iqra! (Soma!)”. Nabii (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “ ما أنا بقارئ (siwezi kusoma)”. Jibraeel (‘alaihis salaam) kisha akamkumbatia na kukaza kumbatio hadi akaanza kusikia maumivu. Kisha akamwachia na kumwagiza tena asome. Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu kwa mara ya pili kwamba hawezi kusoma. Kisha, Jibraeel(‘alayhis salaam) akamkumbatia kwa mara ya pili na kumkandamiza kifuani mwake. Baada ya hapo akamwachia na kusema “Iqra!”
Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu kwa mara ya tatu kwamba alikuwa hawezi kusoma. Jibraeel (‘alayhis salaam) akamkumbatia kwa mara ya tatu kisha akazisoma Aya hizi tano. Ilikuwa ni wakati huu ambapo Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alibarikiwa na nubuwwah (utume).
Baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na Jibraeel (‘alayhis salaam), Nabi (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alirejea nyumbani na alikuwa katika hali ya wasiwasi kuhusu jinsi atakavyotimiza utume. Alimueleza khadija (Radhiya allahu ‘anha) tukio zima la kukutana na Jibreel (‘alayhis salaam) na kumuelezea wasiwasi wake. Khadijah (Radhiya Allaahu ‘anha) alimfariji na kumhakikishia kwamba msaada wa Allah Ta‘ala uko pamoja naye kwa sababu ya sifa tukufu alizokuwa nazo.
Akamwambia: “Hapana! Zikubalie bishara (za Allah Ta’ala). Wallahi! Allah Ta’ala hatokudhalilisha kamwe, Wallahi wewe ndiye unayedumisha mafungamano mema na familia yako, unasema ukweli daima, unabeba mzigo wa wenye shida, unamchumia kwa asiyekuwa na kazi na mali, unawapa wageni ukarimu na kusaidia wanaopatwa na misiba ya asili na misiba.” (Saheeh Bukhari #4953)
Kwa kufarijiwa na Khadijah (Radhiyallahu ‘anha),Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alijisikia faraja na uhuru. Khadijah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa mtu wa kwanza kusilimu mikononi mwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam).
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
Soma kwa jina la mola wako ambaye ameumba (kila kitu). Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu.
Mwanzo wa surah hii, Allah Ta’ala anamwamuru Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuanza kisomo chake kwa kuchukua jina la Allah Ta’ala. Kwa hivyo, tunaposoma Qur-aan tukufu, tunapaswa kuanza kwa kusoma “Bismillahir Rahmaanir Rahim”.
Katika aya hizi, Allah Ta’ala amemtambulisha mwanadamu Kwake na kumfahamisha kuwa Yeye ndiye Muumbaji wa kila kitu. Allah Ta’ala pia amemkumbusha mwanadamu asili na mwanzo wa duni. Asili ya mwanadamu ni pande chafu la damu, lakini Allah Ta‘ala amembariki kwa sura bora na uwezo mzuri, na akampa uwezo wa kuendelea mpaka awazidi hata malaika katika uchamungu.
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
Soma, na Mola wako ni Mwingi wa Rehma.
Katika Aya hii, Allah Ta’ala Anatoa amri ya kusoma kwa mara ya pili, pamoja na kutaja kwamba Yeye ni Mwingi wa Rehema. Katika hili, Allah Ta’ala anatoa ishara ya kwamba ni kwa neema yake tu ndipo mtu ataweza kusoma Qur-aan na kumkumbuka.
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
Ambaye amemfundisha (mwanadamu) kwa njia ya kalamu. Alimfundisha mwanadamu asiyoyajua.
Allah Ta’ala amemfundisha mwanadamu matumizi ya kalamu ambayo ataweza kuendelea katika dini na kumfikia Allah Ta’ala. Hata hivyo, kama vile Allah Ta’ala amemfundisha mwanadamu kupitia njia ya kalamu, Anaweza pia kumfundisha mwanadamu bila kalamu. Basi, Allah Ta’ala amembariki mwanadamu kwa uwezo mbali mbali wa kuona, kusikia na ufahamu ambao kupitia kwao anapata elimu na kufikia mahitimisho sahihi.
كَلّا إِنَّ الإِنسانَ لَيَطغىٰ ﴿٦﴾ أَن رَاهُ استَغنىٰ ﴿٧﴾ إِنَّ إِلىٰ رَبِّكَ الرُّجعىٰ
Kwa hakika, mwanadamu amekiuka mipaka yote, kwa sababu anajiona kuwa yuko huru.
Pamoja na kwamba Allah Ta’ala amembariki mwanadamu kwa uwezo mbali mbali ambao kupitia kwao anapata ufahamu, anasahau kwamba Allah Ta’ala ndiye Mwenye jukumu la kumneemesha kwa neema zote anazozipata. Anaanza kuhusisha mafanikio yote anayoyafurahia kwa juhudi zake binafsi na kumsahau kabisa Allah Ta‘ala. Kwa hivyo, anaishi maisha yanayolingana na vitu yeye anavyovitaka na matamanio yake na kuvuka mipaka yote.
Kwa namna hii, Allah Ta‘ala anaeleza kwamba sababu kuu ya mwanadamu kuvuka mipaka yote na kumuasi Allah Ta’ala ni kwamba mwanadamu anajiona kuwa yuko huru. Anahisi kwamba wakati ana mali na uwezo, basi kwa nini amsikilize mtu yeyote? Kama tu mwanadamu anakumbuka mwanzo wake dhaifu na mnyenyekevu na hapotezi neema ya Allah Ta’ala juu yake, atabakia kwenye njia ya uongofu na utiifu.
Mtu ambaye Allah Ta’ala anamtaja katika Aya hii, ambaye anajiona kuwa ni mtu huru na amevuka mipaka yote, ni Abu Jahl. Licha ya Allah Ta’ala kumbariki kwa mali, ushawishi, heshima , alimuasi Allah Ta’ala na akahusisha mafanikio yake yote kwenye juhudi zake binafsi. Licha ya kuwa katika familia ya Rasulullah(sallallahu ‘alaihi wasallam), aliikataa nubuwwah (utume) wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na akafanya kazi kinyume ya Uislamu. Ilikuwa ni kwa sababu ya kiburi na nafsi yake tu kwamba hakutaka kujisalimisha mbele ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), na kwa hivyo pitisha mipaka yote.
إِنَّ إِلىٰ رَبِّكَ الرُّجعىٰ ﴿٨﴾
Hakika marejeo ni kwa Mola wako.
Katika aya hii, Allah Ta’ala anamkumbusha mwanadamu kwamba siku moja, atafariki na atalazimika kurejea kwa Allah Ta’ala. Mwisho tuu, itambidi atoke kwenye makazi haya ya dunia na kurejea kwenye makazi ya milele ya Akhera ambapo atalazimika kutoa hesabu ya matendo yake. Mwanadamu anaiweka akilini Akhera na kuogopa hisabu ya Akhera, atabakia kwenye njia iliyonyooka.
أَرَءَيتَ الَّذى يَنهىٰ ﴿٩﴾ عَبدًا إِذا صَلّىٰ ﴿١٠﴾ أَرَءَيتَ إِن كانَ عَلَى الهُدىٰ ﴿١١﴾ أَو أَمَرَ بِالتَّقوىٰ ﴿١٢﴾ أَرَءَيتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلّىٰ ﴿١٣﴾ أَلَم يَعلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرىٰ ﴿١٤﴾
Je, umemuona (Abu Jahl) ambaye anamsmamisha, mja (Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)) anaposimama katika Swalaah? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (mja – Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)) yuko juu ya uongofu, au anaamrisha kwa uchamungu (basi vipi Abu Jahl atamzuia)? Unaniambia kwamba ikiwa yeye (Abu Jahl) atakataa na akageuka – hatambui kwamba Allah Ta’ala anaona kila kitu?
Katika aya hizi, Allah Ta’ala anamsifu Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na anatangaza kuwa yeye yuko kwenye njia ya uongofu, anaamrisha watu kwa haki na taqwa.
Kumhusu Abu Jahl, basi Allah Ta’ala Anamhukumu vikali kwa kukanusha haki, kujitenga na Uislamu na kumzuia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kumuabudu Allah Ta’ala. Allah Ta’ala anaeleza kuwa anapomuona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) anaswali, hukasirika na angefanya jitihada za kumzuia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuswali mbele ya Allah Ta’ala.
Kuna wakati mmoja, Abu Jahl alimuona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akiswali katika Haram. Alikasirika sana na akamwambia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), “Je, sikukuonya usiswali? Nikikuona unaswali tena, nitakukanyaga shingo yako!”
Kwa hivyo, Allah Ta’ala anamhakikishia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwamba hatamruhusu Abu Jahl kumfikia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na kutekeleza nia yake potofu kwa sababu Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) yuko katika ulinzi wa Allah Ta’ala.
Allah Ta’ala anasema: “Je, yeye (Abu Jahl) hatambui kwamba Allah Ta’ala anamuona?” Katika hili ni dalili kwamba Allah Ta’ala atamshughulikia Abu Jahl ipasavyo na kumwadhibu.
كَلّا لَئِن لَم يَنتَهِ لَنَسفَعًا بِالنّاصِيَةِ ﴿١٥﴾ ناصِيَةٍ كـٰذِبَةٍ خاطِئَةٍ ﴿١٦﴾ فَليَدعُ نادِيَهُ ﴿١٧﴾
Bali ikiwa (Abu Jahl) hataacha (maovu yake), tutamburuta kwa kisogo, kisogo cha uwongo mpotovu. Basi na aliite baraza lake, nasi tutaliita jeshi letu maalumu (la Malaika).Hapana! .Usimtii yeye (Ewe Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam)), na uwe una sujudu na ukaribie (kwa Allah Ta’ala).
Abu Jahl alikuwa ame jaa na kiburi na kujiona kwa sababu ya mali na uongozi wake. Alihisi kwamba alikuwa na msaada wa watu wake, na wakati wowote atawaita, watakuwa mikononi mwake na wito wa kutimiza amri yake. Kwa hivyo, katika aya hizi, Allah Ta‘ala anamuonya Abu Jahl juu ya adhabu kali ya Aakhirah ikiwa atamzuia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuswali. Allah Ta’ala Anasema: “Ni lazima ajihadhari, Bali ikiwa (Abu Jahl) hataacha (maovu yake), tutamburuta kwa kisogo, kisogo cha uwongo mpotovu. Basi na aliite baraza lake, nasi tutaliita jeshi letu maalumu (la Malaika)”. Kwa maneno mengine, Malaika Wetu watamuangamiza na kumsaidia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) dhidi yake. Ikiwa atakusudia kumzuia Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwenye ibaadah zetu, basi Malaika wetu watamvunja vipande vipande.
Imepokewa kwamba katika tukio moja, wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akiwa katika sajdah, Abu Jahl alikwenda kwake kwa nia mbaya ya kuikanyaga shingo lake la baraka. Hata hivyo, alipokaribia, ghafla aligeuka nyuma kwa hofu. Watu wake walipomuuliza sababu ya kugeuka nyuma, hali yeye aliapa kukanyaga shingo la Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam), alisema: “Nilipokaribia niliona handaki la moto na nikaona humo vitu vinavyoruka”. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema kuwa hao ni Malaika, na lau angesogea mbele, wangemvunja vipande vipande.