Tafseer Ya Surah Naba

عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ‎﴿١﴾‏ عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ‎﴿٢﴾‏ الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ‎﴿٣﴾‏ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ‎﴿٤﴾‏ ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ‎﴿٥﴾‏ أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ‎﴿٦﴾‏ وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ‎﴿٧﴾‏ وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ‎﴿٨﴾‏ وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ‎﴿٩﴾‏ وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ‎﴿١٠﴾‏ وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ‎﴿١١﴾‏ وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ‎﴿١٢﴾‏ وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ‎﴿١٣﴾‏ وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ‎﴿١٤﴾‏ لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ‎﴿١٥﴾‏ وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ‎﴿١٦﴾‏ إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ‎﴿١٧﴾‏ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ‎﴿١٨﴾‏ وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ‎﴿١٩﴾‏ وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ‎﴿٢٠﴾‏ إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ‎﴿٢١﴾‏ لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ‎﴿٢٢﴾‏ لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ‎﴿٢٣﴾‏ لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ‎﴿٢٤﴾‏ إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ‎﴿٢٥﴾‏ جَزَاءً وِفَاقًا ‎﴿٢٦﴾‏ إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ‎﴿٢٧﴾‏ وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ‎﴿٢٨﴾‏ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ‎﴿٢٩﴾‏ فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ‎﴿٣٠﴾‏ إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ‎﴿٣١﴾‏ حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ‎﴿٣٢﴾‏ وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ‎﴿٣٣﴾‏ وَكَأْسًا دِهَاقًا ‎﴿٣٤﴾‏ لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ‎﴿٣٥﴾‏ جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ‎﴿٣٦﴾‏ رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ‎﴿٣٧﴾‏ يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ‎﴿٣٨﴾‏ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ‎﴿٣٩﴾‏ إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ‎﴿٤٠﴾‏

Kuhusu nini wanaulizana? Kuhusu tukio kubwa ambalo wanakhtalifiana? La! Hivi karibuni watakuja kujua. Tena, La! Hivi karibuni watakuja kujua. Je! Hatukuifanya ardhi kuwa kama tandiko, na milima kuwa kama vigingi? Na tumekuumbeni wawili wawili, na tukaufanya usingizi wenu kuwa mahali pa kupumzika, na tukaufanya usiku kuwa ni vazi, na tukaufanya mchana kuwa ni wa kuchumia rizki? Na tumejenga juu yenu mbingu saba zenye nguvu; na tumeiumba taa inayo ng’aa (jua), na tumeteremsha kutoka kwenye mawingu maji kwa wingi, na tukatoa humo nafaka na mimea, na mabustani yenye mimea mizuri.

Hakika siku ya uamuzi ni wakati maalumu. Siku litakapopulizwa barugumu na mtatoka kwa makundi. Na mbingu zitafunguliwa na kuwa milango. Na milima itaondolewa kutoka mahali pake (na kuwa udongo) na itakuwa kama sayari. Hakika Jahannamu ni pahali pa kuteswa. (Ni) makazi ya walio asi. Watadumu humo milele, na hawataonja humo chochote chenye ubaridi wala kinywaji isipokuwa maji ya moto yanayo chemka na usaha. (Adhabu hii) ni malipo yanayofaa (yanayolingana na dhambi zao na vitendo vyao)! Hakika wao hawakuwa wakitaraji (kukabili) hisabu. Na walizikadhibisha Ishara zetu kabisa. Na kila kitu (kutokana na vitendo vyao) tumekiandika katika kitabu. Basi onjeni (matunda na matokeo ya vitendo vyenu), wala Sisi hatutakuzidishieni ila adhabu.

Hakika waja wema wana mafanikio makubwa, mabustani na mizabibu, na wake walio lingana nao, na vikombe (vya mvinyo) vilivyojaa mpaka ukingoni. Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo. (Fadhila hii watapata) ni malipo kutoka kwa wao – malipo yaliyokadiriwa, (kutoka kwa) Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, Mwingi wa Rehma. Hakuna yoyote atakayekuwa na uwezo wa kusema Naye, siku ambayo roho (Jibril [‘Alayhis Salaam]) na Malaika watasimama safu safu. Hawatasema isipokuwa Mwingi wa Rehma (Mwenye kurehemu) Amemruhusu, na Atasema yaliyo sawa. Hiyo ndiyo Siku ya Haki, basi anayetaka ashike njia na arejee kwa Mola wake. Hakika tumekuhadharisheni adhabu inayo karibia, siku ambayo mtu atayaona yale yaliyotangulizwa na mikono yake, na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! (yaani. ili nisingelazimika kukabili hesabu na adhabu ya siku hii.)”

About admin

Check Also

Tafseer Ya Surah Lahab

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ‎﴿١﴾‏ مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ‎﴿٢﴾‏ سَيَصْلَىٰ نَارًا …