6. Wakati wa kunywa, mshukuru Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kwa kinywaji ambacho amekupa kwa kusema “alhamdulillah”.
Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) amesema, “Hakika Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) anafurahishwa na yule anayekula chakula, au anakunywa maji, na kumsifu Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala).”
7. Usinywe kutoka upande uliovunjika kwenye kikombe, kwa sababu inawezekana kwamba unaweza kukatwa.
Abu Sa’eed Khudri (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwakataza kunywa kutoka upande uliovunjika kwenye kikombe.
8. Usipulize kwenye kikombe.
Ibn abbas (Radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah alikataza kupumua ndani ya kikombe au kupuliza ndani yake.
9. Ikiwa kinywaji kinashirikiwa na watu wachache, basi baada ya mtu wa kwanza kunywa, anapaswa kumpa kinywaji hicho kwa yule aliye upande wa kulia kwake.
Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba katika tukio moja, maziwa ambayo yalichanganywa na maji kidogo ililetwa kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam). Wakati huo, Beduwi alikuwa ameka upande wa kulia wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), wakati Abu Bakr (Radhiyallahu anhu) alikuwa amekaa upande wa kushoto wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam). Baada ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikunywa, aliimpa Beduwi kunywa na kusema, “yule ambaye yupo upande wa kulia anapaswa kupewa kwanza, na baada yake yule upande wake wa kulia.”
10. Soma Dua ifuatayo baada ya kunywa maji:
اَلْحَمْدُ لِلّٰهِ الَّذِيْ سَقَانَا عَذْبًا فُرَاتًا بِرَحْمَتِهِ وَلَمْ يَجْعَلْهُ مِلْحًا أُجَاجًا بِذُنُوْبِنَا
Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) ambaye alitujalia na maji ya kunywa kwa neema zake, na hakuifanya iwe na chumvi au uchungu kwa sababu ya madhambi zetu.
11. Soma Dua ifuatayo baada ya kunywa maziwa:
اَللّٰهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْهِ وَزِدْنَا مِنْهُ
Ewe Mwenyezi Mungu, tupe Barakah katika maziwa haya na utubariki na zaidi yake.
12. Sukutuwa mdomo wako baada ya kunywa maziwa.
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu