Fadhila za Jumu’ah

Kusamehewa Madhambi Kwa Kuswali Jumu’ah

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Madhambi yaliyotendwa baina ya Jumu’ah mbili, maadamu si madhambi makubwa, yatasamehewa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) (kwa kuswali Jumu’ah zote mbili).

Siku Maalum ya Waumini

Ibnu Abbaas (radhiyallahu anhuma) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Siku hii (ya Jumu’ah) ni Idi ambayo Allah Ta’ala amewapa Waislamu. Mwenye kuja kwa ajili ya Swalaah ya jumu’ah aoge, na ikiwa anayo pafyum (manukato), basi ajipake kiasi, na nakuhimiza kutumia miswak.”


[1] سنن ابن ماجة، الرقم: 1086، وصحيح مسلم بزيادة: “الصلاة الخمس”: 233

[2] سنن ابن ماجة، الرقم: 1098، وقال العلامة البوصري رحمه الله في مصباح الزجاجة 1/132: هذا إسناد فيه صالح ابن أبي الأخضر لينه الجمهور وباقي رجال الإسناد ثقات

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 6

18. Ukiingia kwenye mkusanyiko wenye mazungumzo au majadiliano ya Dini inafanyika, hupaswi kutoa salaam kwa …