Rafiki wa Nabii Musa (alaihis salaam) katika Jannah

Katika Uislamu, kila tendo jema na tendo la haki lina uwezo kumunganisha mtu na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na kumpatia malipo huko Akhera. Hata hivyo, kuna baadhi ya matendo maalum ambayo yana umuhimu maalum mbele ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) na yanaweza kuwa njia ya mtu kupata wema wa dini nzima na wema wa dunia kwa pamoja.

Miongoni mwa vitendo hivi maalum ni kitendo cha kuonyesha wema kwa viumbe na kuwa na fikra ya dini yao.

Kuna matukio mengi katika historia ambayo yanaonyesha jinsi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Alivyowajaalia watu neema maalum na kuyabadilisha maisha yao kutoka katika uovu hadi wema kwa sababu ya kuwaonea huruma viumbe Wake wawe Waislamu, makafiri au hata wanyama.

Hapo chini kuna tukio kuhusu mtu ambaye kwa nje alikuwa mtu wa kawaida tuu, lakini alipata daraja la juu Akhera kwa sababu ya kuwatumikia wazazi wake na kutimiza haki zao kwa upendo na huruma.

Dua aliyoipata kutoka ndani ya mioyo ya wazazi wake ilimfanya special sana mbele ya Allah Ta’ala hadi akawa rafiki wa Nabii Musa (alaihis salaam) katika Jannah.

Imepokewa kwamba katika tukio moja, Nabii Musa alimuomba Mwenyezi Mungu akisema, “Ewe Mwenyezi Mungu! Nionyesheni mwenzangu katika Jannah!” Allah Ta’ala aliikubali dua ya Nabii Musa (alaihis salaam), akamwonyesha mtu fulani na akasema, “Ewe Musa! Nenda kwenye mji fulani, kwa sababu huko ndiko utamkuta mtu huyu ambaye ni mwenzako katika Jannah.”

Nabii Musa (alaihis salaam) akaondoka na akasafiri mpaka akafika kwenye mji ambao Allah Ta‘ala ameutaja. Alipofika mjini, Nabii Musa (alaihis salaam) alikutana na kijana ambaye alikuwa ni mtu ambaye Allah Ta’ala alikuwa amemuonyesha. Kijana huyo alikutana na Nabii Musa (alaihis salaam) na akamsalimia, lakini hakujua kwamba huyu alikuwa Nabii Musa, Mtume wa Allah.

Nabii Musa (alaihis salaam) alijibu salamu yake, na kisha akamuuliza yule kijana kama angeweza kulala nyumbani kwake kama mgeni wake.

Kijana huyo alikubali akisema, “Nina furaha kuwakaribisha kama mgeni wangu. Ikiwa utafurahiya chochote nitakachokupa kula, basi niko radhi kukuburudisha na kukuheshimu. Nabii Musa (alaihis salaam) akajibu, “Nimefurahishwa na chochote utakachonipa.”

Kijana huyo alikuwa mchinjaji wa nyama kibiashara. Kwa hivyo, baada ya kumkubali. Nabii Musa (alaihis salaam) kama mgeni wake, alimpeleka kwenye sehemu yake ya kuchinja na kumuliza asubiri hadi amalize biashara yake kwa siku hiyo.

Wakati Nabii Musa (alaihis salaam) alipokuwa akingoja kwenye duka la kijana huyo, aliona kwamba wakati wowote kijana huyo anapokutana na kipande chochote cha mafuta au uboho wowote, alikuwa akiuweka pembeni na kuihifadhi.

Hatimaye, kijana huyo alipomaliza kazi yake ya siku moja, alimchukua Nabii Musa (alaihis salaam) hadi nyumbani kwake. Alipoingia nyumbani kwake, alitoa mafuta na uboho aliyokuwa ameyaweka pembeni na kuyapika.

Baada ya chakula kuandaliwa, aliingia ndani ya chumba mmoja. Nabii Moosa (alaihis salaam) aliona kwamba katika chumba hiki, kulikuwa na vikapu viwili vikubwa vimetundikwa karibu na bati la nyumba. Kijana akaenda karibu na kikapu kimoja, na kwa umakini wa hali ya juu na upole, aliishusha chini.

Aliposhusha kikapu, Nabii Moosa (alaihis salaam) aliona kwamba ndani yake alikuwa baba yake ambaye alikuwa mzee sana. Kijana akamtoa baba yake kwenye kikapu na kuosha uso wake. Kisha akafua nguo yake na kuipaka manukato, kisha akamvisha baba yake mavazi safi, yenye harufu nzuri.

Baada ya hapo, alichukua mkate, akaukata vipande vidogo na akaumwagia baadhi ya mafuta yaliyopikwa na uboho juu yake. Kisha akamlisha baba yake mpaka aliposhiba, kisha akampa maji ya kunywa mpaka akaridhika.

Baada ya kumhudumia mzee kwa namna hii na kumtimizia haja zake, yule mzee alimuombea dua akisema, “Ewe mwanangu! Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Asiiache juhudi yako ya kunijali ipotee, na Akufanye kuwa rafiki wa Nabii Musa bin Imraan katika Jannah!”

Kijana huyo kisha akateremsha kikapu cha pili, na Nabii Moosa (alaihis salaam) akagundua kwamba ndani yake kulikuwa na mama yake kijana ambaye pia alikuwa mzee sana. Kijana huyo alimtunza kama vile alivyomtunza baba yake.

Baada ya kumhudumia na kuona mahitaji yake, alimuombea dua wakisema, “Alhamdulillah! Ewe mwanangu! Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Asiiache juhudi yako ya kunijali ipotee, na Akufanye kuwa rafiki wa Nabii Musa bin Imraan katika Jannah!”

Wakati Nabii Musa (alaihis salaam) alipoona kiwango cha huruma na utunzaji ambacho kijana huyo alionyesha kwa wazazi wake wazee, aliingiwa na huruma. Kwa hiyo, akaanza kulia, na katika hali hiyo, akaondoka nyumbani kwa kijana huyo.

Kumwona Nabii Musa (alaihis salaam) akiondoka, yule kijana mara moja akamfuata kwa vile alikuwa mgeni wake, akampa baadhi ya chakula alichokuwa ametayarisha.

Hata hivyo, Nabii Musa (alaihis salaam) akamwambia, “Ewe ndugu yangu! Sina haja ya chakula chako! Sababu pekee ya mimi kuja kwako ni kwamba nilimuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Anionyeshe mwenzangu katika Jannah, na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) akanionyesha kuwa wewe ndiye utakayekuwa mwenzangu katika Jannah.”

Kijana huyo alimuuliza Nabii Musa (alaihissalaam), “Mwenyezi Mungu akurehemu! Niambie wewe ni nani?” Nabii Musa akajibu, “Mimi ni Nabii Musa bin Imraan.” Kusikia hivyo, kijana huyo alishangaa sana hadi akaanguka chini na kupoteza fahamu.

Baada ya kupata nafuu na kupata fahamu, yule kijana aliingia nyumbani kwake na kuwapa wazazi wake habari njema kwamba
Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Amekubali dua yao ya yeye kuwa rafiki wa Nabii Musa (alaihis salaam) katika Jannah.

Aliwaambia kwamba mtu aliyekuwa pamoja naye si mwingine alikuwa ni Nabii Musa (alaihis salaam) mwenyewe, na alikuwa amefikisha habari hizo kwake, kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Mwenyewe, kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) amekubali dua yao.

Waliposikia habari hizo njema, wazazi hao walifurahi sana na wakafariki hapo hapo. Baada ya kuwaogosha maiti, Nabii Musa (alaihis salaam) akaswali swala ya janaazah. Baada ya hapo, kijana huyo alijiunga na Nabii Moosa na kubaki katika kampuni yake hadi mwisho wa maisha yake.

Katika tukio hili, tunaona kwamba sababu ya kijana huyu kubarikiwa kuwa sahaba wa Nabii Musa (alaihis salaam) katika Jannah ni kwamba alikuwa amepata dua za dhati za wazazi wake kwa sababu ya kuwatumikia, kuwa mtiifu kwao na kuwaonyesha wema, upendo na huruma.

Tukiwahudumia pia wazazi wetu tutimize haki zao na kuwatendea upendo na huruma, basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Atatubariki pia kwa kukubalika.

Urithi Ya Watoto Wachamungu

Baba yake Nabii Yunus (alaihis salaam) alikuwa mtu mchamungu akiitwa Mattaa. Yeye na mkewe, kwa muda mrefu, walitamani kwamba Allah Ta’ala Awajaalie mtoto wa kiume na amweke kuwa Nabii wa Bani Israa’il.

Miaka mingi ilipita, huku wakiendelea kuomba dua, mpaka hatimaye, waliamua kwenda kwenye chemchemi iliyobarikiwa ya Nabii Ayyoob (alaihis salaam) na kuoga humo na akapewa shifaa kamili na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)

Wote wawili walikwenda kwenye chemchemi na kuoga maji yake. Baada ya hapo,
walijishughulisha na Swalah na wakamuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) awajaalie mtoto aliyebarikiwa ambaye atakuwa Nabii wa Bani Israa’il.

Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) Akaikubali dua yao na mke wa Mattaa baada ya hapo akashika mimba ya Nabii Yunus.

Baada ya miezi minne ya ujauzito, wakati mtoto alikuwa bado tumboni, Mattaa alifariki dunia na kuiacha dunia hii.

Ingawa Mattaa hakuishi kuona matunda ya dua yake yakitimia, aliacha mwana mchamungu kama urithi wake ambao utaendelea kumpatia thawabu kubwa huko Akhera.

Uwekezaji Wa Akhera

Kutokana na tukio hili, tunaelewa kuwa urithi mkubwa zaidi ni urithi wa kizazi cha watu wema. Urithi huu ni kwamba hautamfaidisha mtu katika dunia hii tu, lakini faida yake itaendelea hadi Akhera.

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mtu anapofariki, vitendo vyake vyote hukatika isipokuwa kwa vitendo vitatu; Sadaqat-ul jaariyah (matendo yake mema ambayo thawabu zake zinaendelea baada ya kufariki kwake), elimu yake ambayo watu wananufaika nayo (baada ya kufariki kwake) na mtoto mchamungu anayemuombea dua.”

Wasiwasi na Dua ya Manabii (alaihimus salaam) kwa Vizazi vyao

Mtu anapochunguza maisha ya manabii (alaihimus salaam), Maswahaba (radhiyallahu anhum) na wachamungu wa zamani, atakuta kwamba waliomba dua maalum kwa ajili ya watoto wachamungu ambao watakuwa urithi kwao baada ya kufariki kwao.

Vile vile, walikuwa na wasiwasi juu ya maendeleo ya deeni cha kizazi chao katika maisha yao yote. Hivyo, Quraan Majeed inataja dua maalum ya Ibrahim na Zakariya (alaihimas salaam) kupata watoto wachamungu.

Vile vile, wakati Ya’qub (alaihis salaam) alipokuwa amelala kwenye kitanda chake cha mauti, aliwausia watoto wake kubaki imara katika Dini baada ya kufariki kwake. Wasiwasi wake mkubwa, hata alipokaribia mwisho wake, ulikuwa kwa ajili ya usalama wa deeni ya kizazi chake baada yake.

About admin

Check Also

Tukio La Mchamungu, Abdullah Bin Marzooq

Abdullah bin Marzooq (rahimahullah) alikuwa mja mchamungu wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aalah)na alikuwa katika zama …