Wazazi Wakiongoza Kwa Mfano

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa mtu bora zaidi katika waja wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala). Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) alimchagua kama mjumbe wake wa mwisho na akambariki na Dini bora zaidi – Dini ya kiislamu ambayo ni kanuni kamili ya maisha kwa mwanadamu kufuata.

Mtu akichunguza tabia uliobarikiwa wa Rasulullah, basi atagundua kuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) alimfanya awe na kiwango cha juu cha tabia na heshima ili aweze kuhudumia kama mfano wa mwisho kwa binadamu kuiga hadi mwisho wa wakati.

Kwa hivyo, kila mwelekeo wa maisha ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ulikuwa ni mfano na bora. Iwe nyumbani, wakati wa kuishi kama mume na mke wake na kuwa baba kwa watoto wake, au iwe msikitini, kama Imamu wa jamaa, au katika jamii kama kiongozi wa Waislamu, alijishika kwa njia kamilifu zaidi na kuwa na kiwango bora kwa watu wote kwa kumfuata.

Kwa hivyo, katika malezi ya mtoto, mpaka na isipokuwa wazazi kuishia kwa kufata maisha na tabia ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), kuleta Sunnah yake katika maisha yao na nyumbani, hawataona na kufikia matokeo yanayotarajiwa katika malezi ya mtoto wao.

Kumfundisha mtoto tu kwa kumpa elimu ya Kiisilamu na kumshauri kwa maneno juu ya maadili mazuri hayatokuwa na athari kubwa kama vitendo vya wazazi, mwenendo na mtindo wa maisha yao unapingana na maneno yao.

Fanya Yale Unachohubiria

Wakati mtu anasoma maisha ya maswahaabah (radhiyallahu anhum) na jinsi walivyofundisha watoto wao na kuwaelekeza kuelekea maadili mema, sifa hii nzuri ambayo inasimama ni kwa sababu walifanya kile walichohubiri na matendo yao yalikuwa ushahidi wa maneno yao.

Pamoja na wazazi wanaoongoza maisha ya uchamungu, na hivyo kuwa mfano mzuri kwa watoto wao, wanapaswa pia kufundisha watoto wao kutimiza haki za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) na haki za Allah Ta’ala.

Wanapaswa kuwaongoza kuhusu usafi wa mdomo, mwili na roho, na msisitizo mkubwa unapaswa kuwekwa juu ya mwenendo wa kijamii na adabu. Wakati Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwafundisha maswahaabah Dini, mafundisho yake yalikuwa kamili na kufunika vipimo vyote vya maisha ya wanadamu.

Anas (Radhiyallahu anhu) akibaki katika Huduma wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam)

Anas (radhiyallahu anhu) alikuwa mhudumu maalum wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ambaye aliheshimiwa na fursa ya dhahabu ya kumtumikia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa miaka kumi hadi kufariki kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).

Katika kipindi hiki cha miaka kumi, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alishiriki naye kwa upendo na akamfundisha Dini. Anasema, “Nilimtumikia Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa miaka kumi. Katika kipindi hiki, hakuwahi kunipiga wala kuzungumza nami kwa ukali, akunikemea, au hata kunitazama kwa jicho baya.”

Kati ya ushauri wa dhahabu na mafundisho ambayo Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliimpa kwake ni yafuatayo:

Elimu kuhusu kutimiza haki za Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) na Viumbe.

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alimuambia Anas (Radhiyallahu anhu), “Ewe mtoto wangu mpendwa! Weka siri zangu, na utakuwa mwamini wa kweli.”

Anas (Radhiyallahu anhu) anasema, “Baada ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kunipa ushauri huu, sikuwahi kutowa siri zake kwa mtu yoyote, licha ya mama yangu na wake wanaoheshimiwa wa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) wakiniulza ni Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ameniambia (wakati hawakujua kuwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alichokuwa ameniambia ilikuwa ya siri.) ”

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) pia alisema, “Ewe mwanangu mpendwa! Ikiwa unaweza Kunitumia salaa na salaam kila wakati juu yangu basi fanya hivyo, kwa sababu malaika watakuombea kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) Kwa msamaha wako. ”

Elimu Kuhusu Kutimiza Haki Za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) kwa kuswali

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alimuambia Anas (Radhiyallahu anhu), “Ewe mtoto wangu mpendwa! Jaribu kuswali (nafl) nyumbani kwako pia. Ewe anas! Unapofanya ruku, basi hakikisha kuwa unashika magoti yako kwa nguvu, na uweke viwiko vyako vyamkono mbali pembeni.

“Ewe mtoto wangu mpendwa! Unapoinua kichwa chako kutoka Ruku, achilia miguu yako yote kutulia na kuwa na utulivu (kabla ya kwenda kwenye Sajdah), kwa sababu siku ya kuhukumu, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) hatomtazama kwa huruma yule ambaye hahunyooshi mgongo wake wakati anasimama kutoka Ruku.

“Ewe mtoto wangu mpendwa! Unaposujudu, weka kichwa chako na Viganja vyako juu ya ardhi vizuri, na usisujudu kwa haraka sana kama jinsi jogoo akitumia mdomo wake kuchukuwa kitu chini, na usilaze mikono yako chini ukisujudu, mkao wakufanana na mbwa au mbweha. Jiepushe na kutazama vitu ukiwa katika Swalaah, kwa sababu kufanya hivyo ni njia ya kuharibu (thawabu ya) Swalaah yako. ”

Elimu Kuhusu Mwenendo wa Kijamii na Kuwa na Dhana Nzuri Kwa kila Mwislamu

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alimuambia Anas (Radhiyallahu anhu), “Ewe mwanangu mpendwa! Unapotoka nyumbani kwako, basi toa salaam kwa kila Mwislamu ambao unamuona, kwa kuwa ikiwa utafanya hivyo, utarudi nyumbani kwako hali ya kwamba dhambi zako ndogo zimesafishwa.

“Ewe mwanangu mpendwa! Unapoingia nyumbani kwako basi toa Salaam kwa familia yako nyumbani. ”

Katika hadithi moja, Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Unapoondoka nyumbani kwako, basi ukimuona Mwislamu yoyote, unapaswa kuhisi moyoni mwako kuwa yeye ni bora kuliko wewe.”

Elimu Kuhusu Kulea Watoto

Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Siku ya saba baada ya mtoto kuzaliwa, aqeeqah inapaswa kufanywa, anapaswa kupewa jina la Kiisilamu na kichwa chake kinapaswa kunyolewa.

“Wakati mtoto anafikia umri wa miaka saba, anapaswa kufundishwa adabu na tabia za Kiisilamu. Wakati anapofikia umri wa miaka tisa, kitanda chake kinapaswa kutengwa na ndugu zake. Wakati anafikia umri wa miaka kumi na tatu, anapaswa kuwa na nidhamu na kupigwa ikiwa haswali au hafungi.

“Wakati anafikia umri wa miaka kumi na sita au kumi na saba, baba yake anapaswa kumuozesha. Baada ya hapo, baba yake anapaswa kumshika mkono wake na kumwambia akisema, ‘Nimekufundisha adabu za Kiisilamu, nimekuelimisha Dini na nimekuozesha. Namuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’ala) akuepushe na Fitnah na imtihani kwangu katika ulimwengu huu na kuwa sababu ya adhabu
Kwangu mimi Akhera.”

Elimu kuhusu kushikilia kila Sunnah na njia ya kuingia Jannah

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alimuambia Anas (Radhiyallahu anhu), “Ewe mwanangu mpendwa! Ikiwa unaweza kutumia mchana wako na usiku bila kuwa na chuki na mtu yoyote moyoni mwako, basi fanya hivyo, kwa sababu hii itafanya Hesabu yako (kuulizwa katika mahkama ya Mwenyezi Mungu) kuwa rahisi.”

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) piaalisema, “Ewe mwanangu! Hii (yaani kuweka moyo wako safi wakati wote) ni Sunnah yangu. Yule anayependa Sunnah yangu ananipenda, na yule anayenipenda atakuwa nami katika Jannah. Ewe mtoto wangu mpendwa! Ikiwa unafuata ushauri wangu huu basi hakutakuwa na kitu kinachopendwa zaidi kuliko kifo. ”

Kutokana na kisa hii, tunaweza kuelewa umuhimu mkubwa wa kuumpa mtoto dini na uelewa wa Dini, kwa njia ya upendo, upole na ya huruma jinsi Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alitumia wakati wa kumfundisha Anas (Radhiyallahu anhu). Pindi mtoto anafundishwa Dini kwa upendo na utunzaji kama huo, atakuwa na shauku na hamu ya Dini moyoni mwake, na baadaye ataishi maisha yake kulingana na maagizo ya dini.

About admin

Check Also

Kumtambulisha Mtoto Kwa Allah Ta’ala

Malezi kwa mtoto ni muhimu sana na inaweza kufananishwa na msingi wamjengo. Ikiwa msingi wamjengo …