Kumswalia Nabii wa Allah ta’ala Mara elfu moja siku ya ijumaah

عن أنس بن مالك قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي في يوم الجمعة ألف مرة لم يمت حتى يرى مقعده من الجنة (أخرجه ابن شاهين بسند ضعيف كذا في القول البديع صـ ٣٩٧)

Ana’s (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema, “Yule ambae atanitumia salaa na salaam mara elfu moja siku ya ijumaah, hato fariki mpaka ameonyeshwa sehemu yake katika jannah.”

Mapenzi ya Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu)  yanaendana na mapenzi ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Sayyidina  Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) aliwahi kumwambia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akisema, “Ingawa nina furaha kwamba baba yangu alisilimu, furaha ambayo ningeipata kwa Uislamu wa mjomba wako Abu Taalib, ingekuwa kubwa zaidi. Sababu ni kwamba kama mjomba wako abu taalib angesilimu, ingekuletea furaha nyingi kwako.”

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …