Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) wakati wa Kuingia na Kutoka Msikitini

عن فاطمة رضي الله عنها قالت: كان رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا دخل المسجد صلى على محمد وسلم وقال رب اغفر لي ذنوبي وافتح لي أبواب رحمتك وإذا خرج صلى على محمد وسلم وقال رب اغفر لي ذنوبي وافتح لي أبواب فضلك (سنن الترمذي، الرقم: 314، وحسنه)

Faatimah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba wakati Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikua akiingia msikitini, alikua akituma salaam na baada ya hapo alikuwa akisoma dua ifuatayo:

رَبِّ اغْفِرْ لِيْ ذُنُوْبِيْ وَافْتَحْ لِيْ أَبْوَابَ رَحْمَتِك

Ewe Mola wangu, nisamehe dhambi zangu na nifungulie milango ya rehema zako.

Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pindi anapotoka msikitini, alikuwa akituma salaam na kisha akisoma dua ifuatayo:

رَبِّ اغْفِرْ لِيْ ذُنُوْبِيْ وَافْتَحْ لِيْ أَبْوَابَ فَضْلِك

Ewe Mola wangu, nisamehe dhambi zangu na unifungulie milango yako za fadhila.

Kubarikiwa na Nguo za Jannah

Sayyidina Sufyaan bin Uyainah (rahimahullah) anaripoti kwamba Khalaf (rahimahullah) amesema:

Nilikuwa na rafiki ambaye nilikuwa nasoma naye Hadithi. Baada ya yeye kufariki, nilimuona katika ndoto kwamba alikuwa akitembea kwa uhuru, akivaa nguo mpya za kijani. Nikamuuliza, “Tulikuwa tunasoma Hadithi pamoja, kwa hivyo uliwezaje kufikia kituo hiki cha juu cha heshima?” Akajibu, “Ndio, tuliandika Hadithi pamoja, lakini kila nilipokutana na jina la baraka la Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam), Nilikuwa nikiandika صلى الله عليه وسلم chini. Kwa malipo ya kitendo hiki, Mwenyezi Mungu amenipa heshima hii unayoiona.” (Al Qawlul Badee, Pg, 486)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …