Maneno Ya Adhaan.

Kuna aina saba ya misemo katika adhaan. Misemo saba ni hizi zimetajwa hapa chini kwa utaratibu maaluum:

1. Kwanza toa Kwa sauti ya juu:

اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ

Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi, Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi.

اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ

Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi, Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi.

2. Pili, taja maneno manne yafuatayo kwa sauti ya chini na kisha toa Kwa sauti ya juu:

أَشْهَدُ أَلَّا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ

Nashuhudia ya kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah subhaana wata’ala.

أَشْهَدُ أَلَّا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ

Nashuhudia ya kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah subhaana wata’ala.

أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَّسُوْلُ اللهْ

Nashuhudia kwamba Sayyiduna Muhammad ni mjumbe wa Allah subhaana wata’ala.

أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَّسُوْلُ اللهْ

Nashuhudia kwamba Sayyiduna Muhammad ni mjumbe wa Allah subhaana wata’ala.

3. Tatu, toa Kwa sauti:

حَيَّ عَلٰى الصَّلَاةْ

Njooni kwenye Swalah.

حَيَّ عَلٰى الصَّلَاةْ

Njooni kwenye Swalah.

4. Nne, toa kwa sauti:

حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ

Njoo kwenye mafanikio.

حَيَّ عَلٰى الْفَلَاحْ

Njoo kwenye mafanikio.

5. Tano, toa kwa sauti:

اَللهُ أَكْبَرَ اللهُ أَكْبَرْ

Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi, Mwenyezi Mungu ndiye mkubwa zaidi.

6. Mwisho toa Kwa sauti:

لَا إِلٰهَ إِلَّا اللهْ

Hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah subhaana wata’ala.

[1] أما احكام المسألة فمذهبنا أن الأذان تسع عشرة كلمة كما ذكر بإثبات الترجيع وهو ذكر الشهادتين مرتين سرا قبل الجهر وهذا الترجيع سنة على المذهب الصحيح الذي قاله الأكثرون فلو تركه سهوا أو عمدا صح أذانه وفاته الفضيلة (المجموع شرح المهذب 3/71)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …