
‘Amr bin Maimoon (rahimahullah) aliwahi kueleza tahadhari kubwa ya Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokuwa akiripoti hadith kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).
Ametaja: “Wakati mmoja, Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alianza kusimulia Hadith kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), aliingiwa na woga na wasiwasi kiasi kwamba jasho lilionekana kwenye paji la uso wake.
Baada ya kusimulia Hadith, alihutubia watu na kusema, ‘Hili ndilo alilotaja Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) au alitaja jambo lililo karibu na hili.” (Al Mustadrak #5374).
Hii ilikuwa ni tahadhari ya hali ya juu ambayo Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliitumia wakati wa kuripoti hadithi ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Aliingiwa na hofu na wasiwasi ili hapaswi kufanya makosa wakati wa kusimulia kutoka kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam), na asikosee kumnasibisha Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) jambo ambalo hakulisema.
Sababu ya khofu yake na wasiwasi wake ni kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) ametaja katika Hadith, “Mwenye kuzua kitu na kuninasibisha nacho, basi anatengeneza makazi yake katika moto wa Jahannam.” (Sahih Bukhaari #107)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu