Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Elimu yake ya Qur-aan Majeed.

Shaqeeq bin Salamah (rahimahullah), mwanafunzi wa Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu), anasimulia kwamba wakati mmoja, Abdullah bin Mas’uud (Radhiyallahu ‘anhu) alitoa khutbah.

Wakati wa khutbah, alitaja, “Na aapa kwa Mwenyezi Mungu!Nimejifunza zaidi ya surah sabini za Quraan Kareem moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam). Na aapa kwa jina la Allah Ta’ala kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanafahamu kuwa mimi ni miongoni mwa wajuzi zaidi wa Qur-aan. Wakati huo huo, sijioni mimi kuwa bora kuliko wote.”

Kwa mujibu wa riwaya moja, Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) pia ametaja, “Lau ningemjua mtu yeyote ambaye ni mjuzi zaidi kuliko mimi (kuhusu Qur-aan Kareem), basi ningesafiri kwenda kwake kupata elimu kutoka kwake.”

Shaqeeq bin Salamah (rahimahullah) ametaja, “(Baada ya khutbah hii), nilikwenda na kuketi kwenye mikusanyiko ya Maswahabah wengine (Radhiyallahu ‘anhum) ili nisikilize watakachosema (kuhusu khutbah ya Abdullah bin Mas’uud (radhiya Allaahu ‘anhu)). Sikumsikia hata mmoja wao akikataa au kukanusha aliyoyasema.” (Sahih Bukhaari #5000, Sahih Muslim #2462, Fathul Baari 48/9)

About admin

Check Also

Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) akiwa na yaqeen na Maneno ya Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Wakati fulani, katika kipindi cha ukhalifa wake, Uthmaan (Radhiyalhu ‘anhu) alikuja kumtembelea Abdullah bin Mas’uud …