Elimu Kuu ya Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma)

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anasema:

Baada ya kifo cha Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), nilimwambia mmoja wa marafiki zangu wa Answaari, “Njoo twende tukajifunze (elimu ya Dini) kutoka kwa maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum), na wengi wao bado wako miongoni mwetu.”

Akaniambia, “Ewe Ibnu Abbaas! Naapa kwa Mwenyezi Mungu, ninashangaa kwamba unadhani watu watahitaji kukurejelea (katika mambo ya deeni) na hawa Maswahaba wakubwa wapo miongoni mwetu!”

Licha ya kauli ya rafiki yake, Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) hakukatishwa tamaa kwa namna yoyote na kutafuta Ilm kwake. Akasema:

Bali niliendelea kutafuta elimu na nikaanza kumwendea kila Sahaabi (aliyesikia hadith kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)).

Kwa njia hii, Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliweza kukusanya kiasi kikubwa cha ilm kutoka kwa maswahaabah (radiyallahu ‘anhum). Akasema zaidi:

Nikimtembelea Sahaabi yoyote (Radhiya Allaahu ‘anhu), nikimkuta amepumzika, basi nilitandaza kitambaa changu kwenye mlango wa nyumba yake na nikimsubiri atoke nje ya nyumba yake. Wakati fulani, uso wangu na mwili wangu wote ungefunikwa na vumbi nikingoja nje ya nyumba yake.

Hata hivyo, hili halikumkatisha tamaa Ibnu Abbaas na juhudi zake za kutafuta elimu na aliendelea kubaki ameketi pale, akingojea kwa shauku swahaba atoke Anataja:

Sahaabi alipokuwa akitoka nyumbani kwake baada ya kupumzika na akiniona, alikuwa akisema: “Ewe binamu yake Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa nini umekuja kwangu? Kusikia hivyo, nilijibu, “Hapana! Ni sahihi zaidi kwangu kuja kwako (kwa sababu mimi ni mwanafunzi na wewe ni ustaad)!”

Abdullah bin Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) hivyo aliendelea na harakati zake mpaka ikafika wakati ambapo watu walianza kumiminika kwake kwa ajili ya kujifunza elimu ya dini. Anasema:

Rafiki yangu wakianswaari aliishi hadi wakati aliposhuhudia watu wakinufaika na elimu yangu (wakati huo, alitambua nilichokuwa nimekifanya kilikuwa kitu bora zaidi), na hivyo akasema, “Mtu huyu hakika amejidhihirisha kuwa ana akili zaidi kuliko mimi.” (Mustadrak Haakim #363)

About admin

Check Also

Dakika za Mwisho za Mu’aaz bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Ulimwengu huu

  Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kufa kwa tauni kafa kama shaheed. Wakati wa …