Kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya kusoma Dua

عن عبد الله بن مسعود قال إذا أراد أحدكم أن يسأل فليبدأ بالمدحة والثناء على الله بما هو أهله ثم ليصل على النبي صلى الله عليه وسلم ثم ليسأل بعد فإنه أجدر أن ينجح (المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 8780، ورجاله رجال الصحيح إلا أن أبا عبيدة لم يسمع من أبيه كما في مجمع الزوائد، الرقم: 17255)

Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) amesema “Wakati wowote mtu kati yenu akikusudia kumwomba Allah (subhaana wata’ala), Basi aanze dua yake kwa kumhimidi na kumtakasa Allah (subhaana wata’ala) kwa sifa zinazostahiki Utukufu na heshima yake. Kisha atume salaa na salaam juu ya Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na baada ya hapo aombe dua, Kwa sababu (kupitia kufuata njia hii ya kuomba dua) kuna uwezekano mkubwa kwamba atakuwa amefanikiwa (katika dua yake kujibiwa).”

Ummu Sulaym (radhiyallahu ‘anha) na Jasho la Barakah la Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Ummu Sulaym (radhiyallahu ‘anha) (aliyekuwa Mahram wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) anaeleza kwamba wakati mmoja, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alimtembelea, na akapumzika mchana (mapumziko ya qayloolah) nyumbani kwake. Pindi alikua amelala, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alianza kutoka jasho.

Anaeleza kwamba alichukua chupa ndogo na kuanza kukusanya jasho lake la baraka. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alipoamka na kuuliza alichokuwa akifanya, alimfahamisha Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwamba alikuwa akikusanya jasho lake la baraka, kwa sababu hapakuwepo harufu nzuri kuliko hiyo. Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alimruhusu kufanya hivyo na hakupinga kitendo hicho. (Saheeh Muslim, 2332)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …