Fadhila za Mwenye kwenda Msikitini Kutekeleza Swalaah

1. Kufanya udhu nyumbani na kutembea kwenda msikitini kuswali ni njia ya mtu kusamehewa madhambi yake na daraja lake kuinuliwa.

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم من تطهر في بيته ثم مشى إلى بيت من بيوت الله ليقضي فريضة من فرائض الله كانت خطواته إحداهما تحط خطيئة والأخرى ترفع درجة (صحيح مسلم، الرقم: 666)

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kutawadha nyumbani na baada ya hapo kutembea kuelekea kwenye nyumba miongoni mwa nyumba za Allah (subhaana wata’ala) ili akamilishe faradhi ya Allah (subhaana wata’ala), Basi Kwa kila hatua moja anachukuwa, dhambi moja inasamehewa, na kwa hatua inayofuata, atainuliwa daraja moja.”

2. Wanaokuja msikitini ni wageni wa Allah (subhaana wata’ala)

عن عمرو بن ميمون عن عمر رضي الله عنه قال المساجد بيوت الله في الأرض وحق على المزور أن يكرم زائره (المصنف لابن أبي شيبة، الرقم: 35758)

Sayyidina Amr bin Maimoon (rahimahullah) anaripoti kwamba Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu) Alisema: “Misikiti ni nyumba za Allah (subhaana wata’ala) Hapa duniani, na mwenyeji wa nyumba huchukua jukumu la kumheshimu yule anayemtembelea.”

3. Wanao kuja msikitini mara kwa mara wamepewa cheo cha ‘watu wa Allah (subhaana wata’ala’) na watumishi wake makhsusi.

عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول إن عمار بيوت الله هم أهل الله عز وجل (مجمع الزوائد، الرقم: 2030)

Sayyidina Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Amesema: “Ni wale tu wanaotembelea misikiti ndio Watu wa Allah (subhaana wata’ala) (watumishi makhsusi).


[1] قال الهيثمي: رواه الطبراني في الأوسط وأبو يعلى والبزار وفيه صالح المري وهو ضعيف صالح ابن بشير ابن وادع المري بضم الميم وتشديد الراء أبو بشر البصري القاص الزاهد ضعيف من السابعة مات سنة اثنتين وسبعين وقيل بعدها (تقريب التهذيب صـ 271) عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول المسجد بيت كل تقي وتكفل الله لمن كان المسجد بيته بالروح والرحمة والجواز على الصراط إلى رضوان الله إلى الجنة (الترغيب والترهيب، الرقم: 501) قال الهيثمي: رواه الطبراني في الكبير والأوسط والبزار وقال إسناده حسن وهو كما قال رحمه الله تعالى

About admin

Check Also

Sunna Za Msikiti

27. Uwe mtulivu na mwenye heshima ukiwa msikitini, wala usighafilike na kusahau heshima ya msikiti. …