Dua zinasimamishwa hadi kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)

عن عمر بن الخطاب قال: إن الدعاء موقوف بين السماء والأرض لا يصعد منه شيء حتى تصلي على نبيك صلى الله عليه وسلم (سنن الترمذي، الرقم: 486)

Umar (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti, “Dua zinabaki kusimamishwa baina ya mbingu na Ardhi. Dua hazifiki mbinguni hadi salaa na salaam inatumwa juu ya Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) (yaani hakuna dhamana ya kukubalika kwao).

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) Alijitolea kwa kubaki na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) ni Sahaabi maarufu wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Hakuna Sahaabi mwingine ambaye aliripoti hadithi nyingi kama alivyofanya yeye. Alisilimu mwaka wa 7 A.H. Na tangu Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alifariki mwaka wa 11 A.H., alikuwa amekuwa naye kwa muda wa miaka minne tu. Watu walikuwa wakimshangaa jinsi aliweza kukumbuka hadithi nyingi katika muda mfupi kama huo.

Anafafanua hili mwenyewe akisema:

Watu wanashangaa jinsi ninavyosimulia hadithi nyingi. Ukweli ni kwamba ndugu zangu wa Muhaajir walibaki kujishughulisha katika biashara na ndugu zangu wa Ansaar walifanya kilimo chao, wakati mimi nilikuwa na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kila wakati. Nilikuwa miongoni mwa watu wa Suffah. Sikuwa na wasiwasi na kutafuta rizqi, na nilibaki naye Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kila mara, kuridhika na chakula chochote kidogo nilicho nacho. Kuna wakati nilikuwa na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Pindi ambapo amna mtu mwengine alikuwepo.

Niliwahi kumlalamikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kuhusu upungufu wangu wa
kumbukumbu. Akaniambia, Tanua shuka lako. Mimi hapo hapo nikafanya hivyo. Baada ya hapo akafanya ishara kwa mikono yake. kwenye shuka langu na kusema, “Sasa jifunike shuka hii.” Nikaifunika kifuani. Tangu wakati huo, sijasahau chochote ambacho nilitaka kukumbuka.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …