Fadhila za Mwenye kwenda kwenye Msikitini Kutekeleza Swalaah

4. Kuenda msikitini mara Kwa mara ni njia ya usalama kwa Imaan na Dini ya mtu.

عن معاذ بن جبل رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال إن الشيطان ذئب الإنسان كذئب الغنم يأخذ الشاة القاصية والناحية فإياكم والشعاب وعليكم بالجماعة والعامة والمسجد (الترغيب والترهيب، الرقم: 499)[1]

Sayyiduna Mu’aaz bin Jabal (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Hakika Shaitaan ni mbwa mwitu wa mwanadamu (anayemuwinda mtu), kama jinsi mbwa mwitu wa mbuzi anayemkamata mbuzi aliye mbali na kujitenga na kundi. Jiepusha na kuishi kwa kujitenga kwenye tambarare (au kujiepusha na maoni yaliyotengwa) na kushikilia kwa uthabiti wa Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah na kubaki na ummah walio wengi na kushikamana na msikiti.”

5. Kuenda msikitini mara Kwa mara ni dalili ya Imaan.

عن أبي سعيد رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا رأيتم الرجل يعتاد المسجد فاشهدوا له بالإيمان قال الله تعالى إنما يعمر مساجد الله من آمن بالله واليوم الآخر (سنن الترمذي، الرقم: 3093)[2]

Sayyiduna Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Unapoona kwamba mtu anaenda msikitini mara kwa mara basi kuwa shahidi kwa Imaan yake. Allah subhaana wata’ala ametaja ndani ya Qur-aan, ‘Misikiti ya Allah subhaana wata’ala inatembelewa tu na wale wenye Imani kwa Allah subhaana wata’ala Siku ya Mwisho.’”

6. Wale wanaokwenda msikitini gizani wamebashiriwa kupata Noor kamili Siku ya Qiyaamah.

عن بريدة الأسلمي رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال بشر المشائين في الظلم إلى المساجد بالنور التام يوم القيامة (سنن الترمذي، الرقم: 223)[3]

Sayyidina Buraidah Aslami (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Wape bashara wale wanaotembea gizani kwenda Msikitini ya Noor yao Siku ya Qiyaamah.

7. Kila mtu anapokwenda msikitini asubuhi au jioni, Allah subhaana wata’alah Humuandalia sehemu yake katika Jannah.

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال من غدا إلى المسجد وراح أعد الله له نزله من الجنة كلما غدا أو راح (صحيح البخاري، الرقم: 662)

Sayyidina Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kwenda msikitini asubuhi na jioni, basi kila anapoelekea msikitini, Allah humuandalia sehemu yake katika Jannah.


[1] قال المنذري: رواه أحمد من رواية العلاء بن زياد عن معاذ ولم يسمع منه

[2] قال أبو عيسى: هذا حديث حسن غريب

[3] قال أبو عيسى: هذا حديث غريب

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …