Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) kabla ya Kufanya Dua

عن فضالة بن عبيد قال: بينا رسول الله صلى الله عليه وسلم قاعد إذ دخل رجل فصلى فقال: اللهم اغفر لي وارحمني فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: عجلت أيها المصلي إذا صليت فقعدت فاحمد الله بما هو أهله وصل علي ثم ادعه قال: ثم صلى رجل آخر بعد ذلك فحمد الله وصلى على النبي صلى الله عليه وسلم فقال له النبي صلى الله عليه وسلم: أيها المصلي ادع تجب (سنن الترمذي، الرقم: 3476 وقال: هذا حديث حسن)

Fadhaalah bin Ubaid (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba katika tukio moja, pindi Rasulullah sallallahu alaihi wasallam alikuwa amekaa (msikitini), mtu fulani aliingia na kuswali. Baada ya kuswali, mtu huyo aliomba dua akisema, “Ewe Allah subhaana wata’ala! Nisamehe na unifariji na rehma zako!” kumtazama namna mtu huyu alivyoomba dua, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Umeharakisha (kumwomba Allah ta’ala haja zako), Ewe Mtu uliye swali! Baada ya kuswali, unapokaa kuomba dua, anza kwa kumhimidi Allah (subhaana wata’ala) kwa vile anastahiki kusifiwa. Baada ya hapo nitumie mimi salaa na salaam, kisha mfikishie Allah ta’ala haja zako.” Baada ya hapo, mtu mwingine pia akaswali. Baada ya kuswali, alimhimidi Allah (subhaana wata’ala), akamtumia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) salaa na salaam (na kisha akaanza kuomba dua). Kumwangalia mtu huyu (na yeye akishikamana na adabu za dua), Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia, “Ewe mtu uliye swali! Omba dua, kwa sababu dua yako itakubaliwa!”

Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) anapoteza Meno Yake

Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ameumizwa vibaya sana na adui na vipande viwili vya kofia yake vikapenya kwenye uso wake wa Baraka.

Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) na Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) mara moja wakakimbia na kumsaidia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam). Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) akaanza kung’oa vipande vya kofia kutumia meno yake. Wakati kipande kimoja kilipotolewa, alikuwa amepoteza jino moja. Hakujutia kupoteza jino lake, akatumia tena meno yake kung’oa kiungo kingine pia.

Alifanikiwa kuong’oa kipande kingine, basi katika harakati hizo, alipoteza jino jingine. Vipande vilipotolewa, damu ilianza kutoka kwenye mwili wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Malik bin Sinaan (radhiyallahu ‘anhu), baba yake na Abu Said Khudri (radhiyallahu ‘anhu), alilamba damu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa mdomo wake. Kwa hili, Rasulullah alisema, “Moto wa Jahannam hauwezi kumgusa mtu ambaye damu yangu imechanganyika na yake. (Fathul Bari, 7/366)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …