Kuandika Salaa na Salaam Wakati Wa Kuandika Jina Tukufu la Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من صلى علي في كتاب لم تزل الملائكة تستغفر له ما دام اسمي في ذلك الكتاب (المعجم الأوسط للطبراني، الرقم: ١٨٣٥، وسنده ضعيف كما في كشف الخفاء، الرقم: ٢٥١٨)

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kasema, “yoyote atakaye nitumia salaa na salaam kwa kuandika ndani ya kitaabu, Malaika wataendelea kumuombea msamaha kwa niaba yake kama tu jina langu lita baki pale pale kwenye kitaabu.”

Mapenzi Ya Swahaba Mmoja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Swahaba mmoja siku moja alikuja kwa Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na kumuuliza, “Ewe! Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ni lini siku ya Qiyaamah?” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Umefanya maandalizi gani kwa siku hiyo?” huyu swahaba akasema, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), sidai kuwa nina Swalaah nyingi, saumu na sadaqah nyingi upande wangu, lakini mimi nina mapenzi ya Allah (subhaana wata’ala) na Mtume Wake (sallallahu alaihi wasallam) moyoni mwangu.” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Hakika kwenye Siku ya Qiyaamah, utakuwa pamoja na wale unaowapenda.”

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema, “Hakuna kilichowafanya Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) kuwa na furaha zaidi kuliko maneno haya ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam). (Sunnan Tirmizi, 2385)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …