Katika tukiyo la Hudaybiyah, Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameamrishwa na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kujadiliana na Maquraishi huko Makka Mukarramah.
Wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameondoka kwenda Makka Mukarramah, baadhi ya Maswahaba walimwonea wivu Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) kwa kuweza kufanya tawaaf ya Nyumba ya Allah subhaana wata’ala Kwa upande mwingine, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Sidhani kama atatamani kufanya tawaaf bila mimi.”
Wakati Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alipoingia Makkah Mukarramah, Abaan bin Said (radhiyallahu ‘anhu) akamchukua kwenye hifadhi yake na akamwambia: “Unaweza kuzunguka kwa uhuru popote unapotaka. Hakuna mtu hapa anaweza kukugusa.”
Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) alifanya mazungumzo yake na Abu Sufyaan na wengine wa Makkah Mukarramah kwa niaba ya Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na alipokuwa karibu kurejea, Waquraishi wenyewe walimwambia, “Sasa ukiwa humu ndani Makkah Mukarramah, unaweza kufanya tawaaf kabla ya kurudi.” Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Itawezekana vipi nifanye tawaaf (bila ya Nabii Muhammad (sallallahu alaihi wasallam)?”
Jibu hili haikuwafurahisha Maquraish na wakaamua kumzuwiya Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) ndani ya Makkah Mukarramah. Habari imewafikia Waislamu kama Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu) amefariki kishahidi.
Pindi habari hii ilimfikia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), alikula kiapo cha utii kutoka kwa Maswahabah wote kupigana mpaka tone la mwisho la damu yao. Maquraishi walipo fahamu haya, hofu iliwaingia na mara moja wakamwachilia Uthmaan (radhiyallahu ‘anhu). Kupitia tukio hili, tunaona mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Uthmaan (Radhiya Allaahu anhu) kwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam), kwamba hakuwa tayari kufanya Twawaaf bila Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam).