Kupata Rehma Kumi

عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: من صلى علي واحدة صلى الله عليه عشرا (صحيح مسلم،  الرقم: ٤٠٨)

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata’alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi” 

Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) anarudi Madina Tayyibah

Baada ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kufariki, ikawa ni vigumu sana kwa Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) kubaki Madinah Tayyibah. Hii ilikuwa ni kwa sababu ya mapenzi mazito aliyokuwa nayo kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Kubaki Madina Munawwara ilimfanya amkumbuke Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika kila hatua na kila kona. Kwa hiyo aliondoka Madinah Tayyibah na akaamua kupita maisha yake yote akijitahidi katika njia ya Allah Ta‘ala.

Aliwahi kumuona Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akimwambia: “Ewe Bilaal, kwa nini umejitenga nami (yaani hunihudhurii)?” Mara moja akaondoka kuelekea Madinah Tayyibah.

Alipofika hapo, Hasan na Husein (radhiyallahu ‘anhuma) wajukuu wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), walimuomba atoe adhaan. Hakuweza kuwakatalia, kwa kuwa walikuwa vipenzi sana kwake.

Mara tu Adhaan ilipoitishwa, watu wa Madinah Tayyibah walilia kwa ukumbusho wa zama za Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Bilaal (radhiyallahu ‘anhu) aliondoka tena Madinah Tayyibah baada ya siku chache na kufariki dunia huko Damascus mwaka wa 20 A.H.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …