Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaana Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume

عن عبد الرحمن بن عوف رضي الله عنه قال خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فاتبعته حتى دخل نخلا فسجد فأطال السجود حتى خفت أو خشيت أن يكون الله قد توفاه أو قبضه قال فجئت أنظر فرفع رأسه فقال ما لك يا عبد الرحمن قال فذكرت ذلك له فقال إن جبريل عليه السلام قال لي ألا أبشرك إن الله عز وجل يقول لك من صلى عليك صليت عليه ومن سلم عليك سلمت عليه (مسند أحمد، الرقم: ١٦٦٢، وقال البيهقي في الخلافيات ٣/١٤٣ عن طريق لهذه الرواية بنحو هذه الألفاظ :قال أبو عبد الله – رحمه الله -: هذا حديث صحيح)

Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu ‘anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa. Nilienda mbele yake kuangalia kuna kitu gani kimemkuta nabii wa mwenyezi mungu (sallallahu ‘alaihi wassallam). Kisha nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) aliinuwa kichwa chake cha baraka kutoka sajida na aliniuliza kuna tatizo gani, nikamueleza ni khofu yangu juu yako (yaani kutangulia mbele za haq ukiwa kwenye sajida). Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alisema, “(sababu ya kufanya sajida ndefu ilikuwa) jibraeel (alaihis salaam) alikuja kwangu na kusema, ‘si nikupe bashara nzuri allah subhaana wata’alah alivyosema, ‘ yoyote atakae kusalia yaani kumsalia nabii, natuma rehma zangu kwake, na yoyote atakae kutumia salaam, nitatuma utulivu na baraka juu yake huyo mtu.'”

Salaa na Salaam Maluum ya Imaam Shaafi’ee (rahimahullah)

Ibnu Bunaan Asbahaani (rahimahullah) anasema:

Wakati fulani nilimwona Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) katika ndoto na nikamuuliza, “ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), je kuna heshima yoyote maalum Muhammad bin Idrees Shaafi’ee (rahimahullah) kapewa, ambaye ni mtoto wa ‘mjomba wako’? .(‘Mjomba’ ametajwa kwa sababu ukoo wa Imaam Shaafi’ee (rahimahullah) inakutana na kizazi cha Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa Abd Yazid bin Hishaam, ambaye baba yake, Hishaam, alikuwa ndiye babu yake Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Ndiyo hakika nimemuomba Allah ta’ala aokoke na hisabu siku ya Qiyaamah.” Kisha nikauliza, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ni kwa kitendo gani ambacho alistahiki upendeleo huo?” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Ni kwa sababu amenitumia salaa na salaam ambayo hakuna mtu mwingine yoyote aliwahi kunitumia.” Kisha nikauliza, “ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), ni salaa na Salaam gani hiyo?” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu:

اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ كُلَّمَا ذَكَرَهُ الذَّاكِرُوْنَ وَصَلِّ عَلٰى مُحَمَّدٍ كُلَّمَا غَفَلَ عَنْ ذِكْرِهِ الْغَافِلُوْنَ

Ewe Allah ta’ala! Mtumie rahma maluum Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) sawa sawa na idadi ya watu ambao wanamkumbuka, na mtumie rahma maalum Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) sawa sawa na idadi ya watu ambao husahau kumkumbuka). (Tabaqaat Us Shaffe Al Kubra Lis Subki 1/188)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …