Mapenzi ya Umar (radhiyallahu ‘anhu) na Kumbukumbu za Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Usiku mmoja, katika kipindi cha ukhalifa wake, Umar (radhiyallahu ‘anhu), alikuwa kwenye ulinzi wa usalama na aliona mwanga na kusikia sauti ikitoka katika nyumba fulani. Alimkuta bibi kizee ndani yake akisokota pamba na kuimba nyimbo zifuatazo:

عَلَى مُحَمَّدٍ صَلَاةُ الْأَبْرَارْ ** صَلَّى عَلَيْكَ الْمُصْطَفَوْنَ الْأَخْيَارْ

“Wacha Mungu waendelee kutuma salamu kwa Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Na waja wa Allah  walio bora na walochaguliwa zaidi wakuswalie (Ewe Muhammad (sallallahu ‘alaihi wasallam))!

قَدْ كُنْتَ قَوَّامًا بَكِيَّ الْأَسْحَارْ

“Ewe Mtume wa Allah ulisimama katika ibada kila usiku, na ulilia (katika dua kwa ajili ya umma) kabla ya alfajiri ya kila siku.

يَا لَيْتَ شِعْرِي وَالْمَنَايَا أَطْوَارْ ** هَلْ تَجْمَعُنِي وَحَبِيبِي الدَّار

“Laiti ningejua kama nitaunganishwa na mpendwa wangu katika Akhera, kwani kifo huja katika hali tofauti, na sijui nitakufa vipi.”

Aliposikia hizi shairi, Umar (radhiyallahu ‘anhu) aliketi chini, akilia kwa upendo na kumbukumbu wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …