Mapenzi ya Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) na Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) wanaondoka kufanya hijrah usiku. Wakati wa safari, muda mwingine Abu Bakr Siddeeq alitembea mbele ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na kuna muda mwingine akitembea nyuma yake. Kuna wakati fulani alitembea upande wa kulia wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na wakati mwingine upande wa kushoto.

Pindi Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alipoliona jambo hili la ajaabu, aliuliza, “Ewe Abu Bakr! naona ukitembea mbele yangu au nyuma yangu wakati fulani kwa upande wangu. Ni nini kinakufanya kuwa na tabia kama hii?” Abu Bakr Siddeeq (radhiyallahu ‘anhu) akajibu: “Wakati wowote wazo la adui hutokea kwangu kama adui atakufuata kutoka nyuma, basi mimi huenda haraka kuelekea nyuma, na wakati wowote hofu ikinitokea la adui kutokea mbele yako kukudhuru, basi mimi kukimbilia mbele yako. Hivyo hivyo, wakati wazo linapoingia akilini mwangu la adui kushambulia kutoka kulia au kushoto, basi mimi kuelekea uko.”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kisha akasema, “Ewe Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu)! Unapendelea maisha yako kuyatoa muhanga kwa ajili yangu?” Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Ndio kwa uhakika ewe Mtume wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), Ninaapa kwa yule ambaye amekutuma wewe na ukweli wa Uislamu!

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …