Kutuma Salaa na Salaam juu ya Manabii (alayhi mus salaam) Wengine Pamoja na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

عن أنس رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : خرج جبريل عليه السلام من عندي آنفا يخبرني عن ربه عز وجل : ما على الأرض مسلم صلى عليك واحدة إلا صليت عليه أنا وملائكتي عشرا فأكثروا علي من الصلاة يوم الجمعة وإذا صليتم علي فصلوا على المرسلين فإني رجل من المرسلين (فوائد أبي يعلى الصابوني كما في القول البديع صـ 250)

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah sallallahu alaihi wasallam alisema, “Jibreel (alayhis salaam) ametoka kwangu sasa hivi. Amekuja kunifahamisha kwamba Allah ta’ala amesema, ‘Hakuna Muislamu duniani anayetuma salaa na salaam juu yako (yaani juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)) mara moja, isipokuwa kwamba Mimi na Malaika Wangu tutamtumia salaa na salaam juu yake (yaani nammiminia rehema kumi na Malaika wangu wamwombee msamaha mara kumi) kwa hivyo niswalie mara nyingi siku ya ijumaa, na utakapo niswalia, basi tuma salamu kwa Manabii (alayhi mus salaam), kwa sababu mimi ni Nabii miongoni mwa Manabii (alayhi mus salaam).”

Katika Hadith hii, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ametufundisha kwamba wakati wowote tunapotuma salaa na salaam juu yake, tunapaswa kutuma salamu kwa Manabii vile vile. Kwa hivyo, tunapomswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), tunapaswa kuongeza yafuatayo mwishoni:

وَعَلٰى الْمُرْسَلِيْن

Na kwa Manabii (alayhi mus salaam) vile vile.

Waa’il (radhiyallahu ‘anhu) Ana Nyoa Nywele Zake

Waa’il bin Hujar (radhiyallahu ‘anhu) anasema:

Kuna wakati fulani nilimtembelea Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wakati nywele za kichwa changu zilikuwa ndefu sana. Nilipokuwa nimekaa naye, alitamka maneno, “Zubaab, Zubaab” (yakimaanisha kitu kibaya). Nilifikiri kwamba alikuwa akimaanisha nywele zangu. Nilirudi nyumbani na mara moja nikakata nywele zangu.

Siku iliyofuata, nilipoenda kumtembelea tena, alisema, “Sikuwa nikimaanisha nywele zako nilipotamka maneno hayo jana. Hata hivyo, ni vizuri ulinyolewa.”

Kitendo hiki cha Sahaabi (radhiyallahu ‘anhu) kinaakisi upendo wa kweli aliyo nao kwa ajili ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ndani ya moyo wake. Mara tu alipotilia shaka kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa hakupendezwa naye kwa sababu ya nywele zake ndefu, mara moja alinyoa nywele zake. Mtu anaweza kufikiria vizuri ikiwa hii ilikuwa kiwango cha upendo waliyokuwa nao, ambapo kulikuwa na shaka tu juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kukasirika na kuwafanya wawe na wasiwasi, basi ingewezekana kwao kuasi amri ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) au kwenda kinyume na sunna zake? (Sunan Abi Dawood, #4089)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …