Sunna Za Msikiti

14. Hakikisha unazima simu yako ya mkononi unapoingia msikitini ili isilete usumbufu kwa wale wenye
kujishughulisha na kuswali na ibaadaah zingine.[1]

15. Usipige picha au kutengeneza video ukiwa msikitini. Kupiga picha au kutengeneza video za vitu vilivyo hai ni haraam katika Uislamu, na kufanya hivyo katika msikitini ni dhambi kubwa zaidi.

عن عبد الله رضي الله عنه قال سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول إن أشد الناس عذابا عند الله يوم القيامة المصورون (صحيح البخاري، الرقم: 5950)

Sayyidina Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Sayyidina Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Hakika watu watakaoadhibiwa vikali zaidi na Mwenyezi Mungu siku ya Qiyaamah watakuwa ni wale wanaohusika katika upigaji wa picha.”

16. Wakati wa kuzungumza ndani ya msikiti, ni makrooh kuinua sauti yako.[2]

مالك أنه بلغه أن عمر بن الخطاب بنى رحبة في ناحية المسجد تسمى البطيحاء وقال من كان يريد أن يلغط أو ينشد شعرا أو يرفع صوته فليخرج إلى هذه الرحبة (موطأ مالك، الرقم: 602)

Imaam Maalik (rahimahullah) anaripoti kwamba Sayyidina Umar (radhiyallahu ‘anhu) alitayarisha eneo kubwa pembeni kabisa na Msikiti uliokuwa ukiitwa Butaihaa. Akaeleza, “Mwenye kutaka kupiga kelele au kuimba mashairi au kuinua sauti yake wakati wa kuzungumza, basi atoke mahali hapa (mbali na Musjid na azungumze).”

17. Msibishane na yoyote ndani ya msikiti kwa sababu hii inauhalifu utakatifu wa msikiti.[1]


[1] تكره الخصومة في المسجد ورفع الصوت فيه ونشد الضالة وكذا البيع والشراء والاجارة ونحوها من العقود هذا هو الصحيح المشهور (المجموع شرح المهذب 2/141)

[2] كره اللغظ ورفع الصوت في المسجد (إعلام الساجد بأحكام المساجد صـ 326)

About admin

Check Also

Sunna Za Msikiti

27. Uwe mtulivu na mwenye heshima ukiwa msikitini, wala usighafilike na kusahau heshima ya msikiti. …