Kutuma Salaa na Salaam juu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) pamoja na Manabii wengine

عن قتادة عن أنس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إذا صليتم علي المرسلين فصلوا علي معهم فإني رسول من المرسلين ( الصلاة على النبي لابن أبي عاصم، الرقم: 69، وإسناده حسن جيد كما في القول البديع صـ 134)

Imepokewa kutoka kwa Anas (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mnapotuma salaam kwa Manabii, basi nitumieni salaam pamoja nao, kwa sababu mimi pia ni Mtume kutoka miongoni mwa Mitume wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)”

Katika Hadith hii, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ametufundisha kwamba wakati wowote tunapotuma salaam kwa Manabii, tumtumie salaam zake pia. Kwa hivyo, tunapochukua jina la Nabii yoyote, tunapaswa kujaribu kusoma yafuatayo:

عَلَيْهِ وَعَلٰى نَبِيِّنَا الصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ

Amani na salaam zimshukie yeye na Nabii wetu (sallallahu alaihi wasallam) pia.

Upendo Wa Dhati kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Wakati mapatano ya Hudaybiyah yalipokuwa yakijadiliwa, Urwah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu) aliyekuwa mjumbe wa Maquraish (ambaye wakati wa mapatano ya Hudaybiyyah alikuwa bado hajasilimu), alipata fursa ya kushuhudia mwenendo wa Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Aliporudi kwa watu wake aliwaambia:

Nimekuwa kwenye mahakama za wafalme wakuu kama mjumbe. Nimekutana na Wafalme wa Persia, Rumi na Abyssinia. Hakuna mahali popote nimewaona watu kwa mfalme wao wakimuonesha heshima kama nilivyowaona masahaba wa Muhammad (sallallahu alaihi wasallam) wakimuonesha yeye heshima.

Anapotema mate, mate yake ya baraka hawairuhusu kumwagika chini. Inachukuliwa na mtu mikononi mwake na kupaka usoni mwake na mwili wake kwa hayo (ili kupata baraka). Anapotoa amri, kila mtu huharakisha kuitekeleza. Anapofanya wudhu, maswahaba wake hukimbiana ili kuyachukuwa maji yanayotiririka kutoka kwenye viungo vyake, kwa namna ambayo mtazamaji atafikiri kwamba wanapigana juu ya maji hayo. Anapozungumza, kila mtu ananyamaza (kwa heshima). Hakuna mtu anayeinua macho yake kumwangalia, kwa heshima yake. (Saheeh Bukhari, #2731)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …