Allah Ta’ala Akitangaza Radhi Zake kwa Maswahaabah Vipendwa wa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)

Allah Ta’ala anataja ndani ya Qur-aan Takatifu kuhusu Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِين وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَ‌ٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٠٠﴾

Na waliotangulia (katika Dini) katika wa Muhajirina na wa Answaar na waliowafuata kwa wema, Allah Ta’ala ameridhika nao na wao wameridhika naye, na amewaandalia mabustani ambayo mito yanapita kati yake, watakaa humo milele. Huko ndiko kufaulu kukubwa. (Sura Taubah: 100)

Upendo wa dhati na juhudi ya ajabu ambayo Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walionyesha kwa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) inaweza kupimwa kwa urahisi kutokana na uchunguzi na ushahidi wa Makafiri wa wakati huo.

Wakati Mkataba wa Hudaibiyah ulipokuwa ukijadiliwa, Urwah bin Masoud (Radhiya Allaahu ‘anhu), mjumbe wa Maquraish (ambaye baadaye alisilimu), alipata fursa ya kuchunguza kwa makini na kusoma tabia na mwenendo wa maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)

Aliporudi kwa watu wake aliwaambia:

“Enyi Waquraishi! Nimekuwa mjumbe wa wafalme wengi wakuu. Nimeziona mahakama za Kaisari, Wakorori na Negus. Wallahi! hakuna mahali ambapo nimeona watu walio karibu na mfalme au mtawala wakimheshimu sana kama nilivyowakuta maswahaba wa Muhammad (Sallallaahu ‘alaihi wasallam).

“Muhammad (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) akitema mate, wanakimbilia kuchukua mate mikononi mwao kabla hayajagusa chini ya ardhi na kupaka kwenye uso zao na mwili zao kumtumia hayo mate. Anapotoa agizo na amri lolote, wote hukimbilia kulitekeleza.

“Anapofanya wudhu, wanashindana wao kwa wao kuokota tone la maji yaliyotumika kabla hayajaanguka kwenye ardhi. Iwapo mtu yoyote atashindwa kupata maji hayo, basi atagusa mikono iliyolowa ya mtu aliyefanikiwa kuyapata kisha anajipaka mikono yake usoni.

“Wanapozungumza mbele yake, wao huzungumza kwa sauti ya chini na pia hawanyanyui macho yao kumtazama usoni, kwa sababu ya kumheshimu. Nywele zinazoanguka kutoka kichwani au ndevu zake zinahifadhiwa ili wapate baraka kutoka kwake na kisha wanazitunza kwa heshima kubwa.

“Kwa kifupi, sijapata kuona kundi lolote la watu wakimpenda kiongozi wao na kua mtiifu sana kama vile nilivyowaona maswahaba wa Muhammad (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) wakimpenda na kumtii yeye.” (Fazaail- e-Aamaal, Pg 166)

Allah Ta’ala atujaalie upendo wa kweli wa Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) na Maswahaabah zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na atujaalie Tawfiq ya kufata Sunnah Mubaraka zake katika nyanja zote za maisha yetu.

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …