Mapenzi Kwa Maswahaabah

Ja’far As Saaigh (Rahimahullah) anasimulia tukio hili ifuatayo:

Miongoni mwa majirani wa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) alikuwa mtu ambaye alihusika katika madhambi mengi, maovu na vitendo visivyo na haya. Siku moja mtu huyu alikuja kwenye mkusanyiko wa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) na akamsalimia kwa salaam. Ingawa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) alimjibu salamu yake, hakumuonyesha makini na kumpokea kwa mapenzi badala yake, alionekana kukosa raha mbele ya mtu huyu (kwa sababu mtu huyu alijulikana sana kuwa na njia mbaya na tabia za maovu)

Mtu huyo mara moja aligundua usumbufu wa Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahullah) na hivyo akasema, “Ewe Abu Abdillah! kwa nini unasumbuka mbele yangu? kupitia ndoto niliiona nimebadilika kabisa na mimi sio tena yule mtu ulikuwa ukinijua kuwa. Imaam Ahmad (Rahimahullah) akauliza, “Umeona ndoto gani?”

Yule mtu akajibu, “Nilimuona Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto yangu. Ilionekana kama alikuwa kwenye eneo la juu na watu wengi wamekaa chini yake. Mmoja baada ya mwingine, watu walisimama na kumwomba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) kuwaombea dua. Waliposimama na kuomba, Rasulullah akawaombea dua mpaka mimi nikabakia.

“Pia nilitaka kusimama na kumuomba Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) anifanyie dua lakini niliona haya na kujisikia vibaya kufanya hivyo kwa sababu ya matendo zangu maovu na njia zangu mbaya. Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) kisha akanihutubia na kuniuliza, “Ewe fulani bin fulani ! kwanini hausimami na kuniomba nikufanyie dua?” nikamjibu, “Ewe Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) ni aibu na fedheha yangu kwa matendo zangu maovu ndiyo inayonizuia kufanya hivyo.”

“Rasulullah akajibu, “ikiwa ni aibu na fedheha inayokuzuilia, basi simama na uniombe nikufanyie dua. Bado tuu nitakuombea dua, kwa sababu unawapenda Maswahaabah wangu na uwasemagi vibaya”. Basi nikasimama na Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam) aliniombea dua.

“Pindi nilipoamka, nilikuta kwamba Allah Ta’ala amenipandikiza ndani yangu chuki kamili na kuchukizwa kwa madhambi zote nilizoshiriki.”

Imaam Ahmad (Rahimahullah) aliposikia tukio hili, alituhutubia akisema, “Ewe ja’far! Ewe fulani na fulani! Wambie watu kuhusu tukio hili na usilisahau, kwa sababu lina manufaa na kutia moyo kwa watu.”

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …