
Mtu kutoka katika kabila la Banu Sulaym alisimuliya yafuatayo:
“Wakati mmoja nilikuwa nimekaa kwenye mkutano ambao Abu dhar alikuwepo pia. Wazo lilikuwa akilini mwangu kwamba labda Abu dharr amekasirishwa na Uthmaan (Radhiyallahu ‘Anhu) kwa sababu Uthmaan (Radhiyallahu anhu) alimuomba aondoke Madinah Munawwarah na aende kuishi katika sehemu inayoitwa Rabadha.
Wakati wa mkutano huo, mtu alipitisha maoni dhidi ya Uthmaan (Radhiyallahu ‘Anhu). Wakati Abu dhar (Radhiyallahu ‘Anhu) aliposikia maoni mabaya ya mtu huyo kuhusu Uthmaan (Radhiyallahu’ Anhu), mara moja akajibu akisema:
“Usiseme chochote kuhusu Uthmaan (Radhiyallahu ‘Anhu) kama sio mema, kwa maana nilikuwepo sehemu ambapo nilishuhudia kitu maalum kinafanyika na Uthmaan (Radhiyallahu anhu) ambayo sitaisahau.
“Wakati mmoja, niliomba ruhusa ya kuwa na Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) mimi na yeye tu ili niweze kupata faida kwake na kusikia ushauri gani angenipa.
“Baada ya kuwa na Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kwa muda mrefu, Abu Bakr (Radhiyallahu’ Anhu) alikuja kwa Rasulullah (Sallallahu Alaihi Wasallam), akifuatiwa na Umar (Radhiyallahu (Radhiyallahu ‘Anhu) na kisha Uthmaan (Radhiyallahu anhu). Wote walikuja kwa Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam), mmoja baada ya mwingine, kwa muda mfupi kati.
“Wakati sisi sote tulikuwepo na Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam), alichukua kokoto katika mkono wake uliobarikiwa, na kokoto zilianza kusoma Tasbeeh kwenye mkono wake uliobarikiwa. Tasbeeh zilikuwa zinaskika kwa sauti kama sauti ya nyuki. Kisha akakabidhi kokoto kwa Abu Bakr (Radhiyallahu ‘Anhu), na waliendelea kusoma Tasbeeh mikononi mwake. Alipoviweka chini, vilibaki kimya.
“Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kisha akamkabidhi Umar (Radhiyallahu’ Anhu), na vikaanza kumsomea Tasbeeh mikononi mwake pia. Baada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alivichukua kutoka Umar (Radhiyallahu Anhu) na kuviweka chini, vikakaa kimya.
“Baada ya hapo, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alikabidhi kokoto kwa Uthmaan (Radhiyallahu ‘Anhu), na pia vikaanza kusoma Tasbeeh mikononi mwake. Kisha akavirudisha na kuviweka chini, baada ya hapo vikakaa kimya. ” (Siyar A’laamin Nubala 2/453)
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu