8. Usilale juu ya tumbo lako.
Ya’eesh Ghifaari (Radhiyallahu anhu) anaripoti: Wakati mmoja, nilikuwa nimelala kwenye tumbo msikitini kutokana na maumivu ya tumbo. Ghafla, mtu alikuja na kunishtuwa na mguu wake akisema, “Kulala katika hali hii (yaani. juu ya tumbo) haipendezwi na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) (Niligeuka kuangalia ni nani alikuwa anaongea nami, kisha) nikaona kwamba ni Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).
9. Usilale na mwili wako wote uchi au na satr (sehemu za siri) kuonekana. Badala yake, lala umevaa mavazi ambayo huficha satr yako.
Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Abu Muusa Ash’ari (Radhiyallahu anhu) alikuwa akiufunika mwili wake (vizuri) wakati wa kulala ili kuhakikisha kwamba sehemu zake za siri hazionekani.
10. Lala mapema na nia ya kuamka Tahajjud.
Imepokewa kutoka kwa Abud Dardaa (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kulala usiku kwa nia ya kusimama kwenye Tahajjud, na macho yake yakamzidi nguvu mpaka Alfajiri, basi atapata thawabu ya kuswali Tahajjud kutokana na nia yake, na usingizi wake utahesabiwa kuwa nisadaqah (baraka) aliyoipokea kutoka kwa Mola Wake.
11. Usilale bila ya sababu maalum baada ya Maghrib. Ikiwa una hitaji kulala (k.m. kutokana na ugonjwa au uchovu mwingi) basi hakikisha una mtu wa kukuamsha muda wa Esha au weka alarm.
Abu Barzah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa hapendi mtu kulala kabla ya esha (baada ya maghrib) na kushiriki katika mazungumzo baada ya Esha (katika hali ambayo hakuna haja).
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu