3. Kabla ya kulala, unapaswa kungusa kitanda chako, kwa sababu kunaweza kuwa na wadudu wa hatari kwenye kitanda.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Wakati mtu akienda kulala kitandani, basi anapaswa kupangusa kitanda na sehemu ya ndani ya kikoi chake. Sababu ni kwamba mtu hajui kile kinachoweza kuingia kitandani kwake (kama wadudu).”
4. Safisha mdomo wako kwa kutumia Miswaak kabla ya kulala.
Abu Hurairah (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba wakati wowote Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alienda kulala usiku au kuamka usiku, alikuwa akitumia Miswak.
5. Ni Mustahab kutumia Surmah kabla ya kulala.
Abdullah bin Abbaas (Radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “paka wanja kwa kutumia ithmid (aina ya wanja), kwa hakika inasafisha na husababisha nywele (kope) kukua.” Abdullah bin Abbaas (Radhiyallahu anhuma) anasema zaidi kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa na chombo cha wanja ambayo alikuwa akitumia kila usiku. Alikuwa akitumia wanja mara tatu kwenye jicho la kulia na mara tatu katika jicho la kushoto.
6. Soma dua na dhikr kabla ya kulala.
اَللّٰهُمَّ بِاسْمِكَ أَمُوْتُ وَأَحْيٰى
Ewe Mwenyezi Mungu, na jina lako nakufa na kuishi.
7. Kulala upande wa kulia na weka mkono wako wa kulia chini ya shavu lako la kulia.
Hafsah (Radhiyallahu anha) anaripoti kwamba pindi Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alitaka kulala, alikuwa akiweka mkono wake wa kulia chini la shavu lake na akiwa akisoma dua ifuatayo mara tatu:
اَللّٰهُمَّ قِنِيْ عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ
Alislaam Juhudi za Kuleta uislam ndani ya maisha yetu