Kupata Rehma Kumi

عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: من صلى علي واحدة صلى الله عليه عشرا (صحيح مسلم،  الرقم: ٤٠٨)

Sayyiduna Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kuwa Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) amesema ” yoyote atakaye nitumia salaam mara moja, allah subhaana wata’alah atamtumia salaam (yaani atampa zawadi na atamfariji na rehema zake) kwake mara kumi” 

Mapenzi Makubwa ya Maswahaba (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah sallallahu alaihi wasallam

Siku moja, mtu mmoja alikuja kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema: “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) mapenzi yangu kwako ni kwamba ninapokufikiria wewe huzidiwa na mapenzi yako, kiasi kwamba sipati kuridhika mpaka nikuone. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), mawazo yananipitia moyoni mwangu kwamba ikiwa Allah ta’ala atanijaalia Pepo, itakuwa vigumu sana kwangu kukuona, kwa sababu utakuwa katika nafasi ya juu ambapo sitaweza kufika.”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamtuliza kwa kumsomea aya ifuatayo katika jibu lake.

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَ وَحَسُنَ أُو۟لَٰٓئِكَ رَفِيقًا

Watu wote wanaomtii Allah subhaana wata’ala na Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) wamo katika kundi la wale ambao juu yao ziko rehema za Allah ta’ala; Manabii, Siddiqin, Mashahidi, na Wachamungu.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …