Swalah Ya Wanaume

Nafasi ya juu ambayo Swalah inashikilia katika maisha ya Muislamu haihitaji maelezo yoyote. Ukweli kwamba kitakuwa ni kipengele cha kwanza ambacho mtu ataulizwa Siku ya Qiyaamah ni ushahidi tosha wa umuhimu wake.

Sayyidina Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) amesema:

إن أول ما يحاسب الناس به يوم القيامة من أعمالهم الصلاة قال يقول ربنا جل وعز لملائكته وهو أعلم انظروا في صلاة عبدي أتمها أم نقصها فإن كانت تامة كتبت له تامة وإن كان انتقص منها شيئا قال انظروا هل لعبدي من تطوع فإن كان له تطوع قال أتموا لعبدي فريضته من تطوعه ثم تؤخذ الأعمال على ذاكم (سنن أبي داود، الرقم: 864)[1] 

Hakika kitendo cha kwanza ambacho watu watahesabiwa Siku ya Qiyaamah ni Swalah zao. Mola wetu atawaambia Malaa’ikah, na hali kwamba Allah ta’ala ana ilimu kamili juu ya kila kitu, “Angalia (fardhi) ya mja wangu; je, ameifanya kwa ukamilifu au ameifanya kwa njia yenye upungufu?” Ikiwa Swalah yake ilitekelezwa kwa ukamilifu, malipo kamili yataandikiwa kwa ajili yake. Ikiwa kulikuwa na upungufu fulani katika Swalaah yake, Allah Ta’ala atawaambia Malaa’ikah, “Fidia upungufu katika swalah yake ya fardh kupitia Swalaah yake ya nafl. Baada ya hapo, ibaadah zingine zitafuata mtindo huo huo.


[1] هذا الحديث سكت عنه أبو داود والمنذري (مختصر سنن أبي داود، 1/306)

About admin

Check Also

Rakaa ya pili

1. Unapoinuka kutoka kwenye sajdah, kwanza inua paji la uso na pua, kisha viganja na …