Wasiwasi wa Mwanamke wa Answaari Kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Katika vita vya Uhud, Waislamu walipata hasara kubwa na idadi kubwa kabisa yao waliuawa. Taarifa nzito zilipofika Madinah Munawwarah, wanawake hao walitoka nje ya nyumba zao wakiwa na shauku ya kutaka kujua undani wa vita hivyo.

Alipouona umati mkubwa wa watu wamekusanyika mahali fulani, mwanamke mmoja waki Answaar aliuliza kwa wasiwasi, “Vipi hali ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)?” Alipoambiwa kuwa baba yake aliuawa vitani, alisema ‘Inna lillahi wa inna ilaihi raaji’uon’ na. kwa kukosa subira alirudia swali lile lile kuhusu Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam).

Wakati huu, aliambiwa kwamba mume wake hayuko tena, kaka yake alikuwa amekufa na kwamba mtoto wake pia aliuawa. Kwa wasiwasi unaozidi kuongezeka, alirudia swali lile lile kuhusu hali ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam).

Aliambiwa kwamba alikuwa salama na mzima, lakini hakutaka kupumzika, na alisisitiza kumwona yeye mwenyewe. Wakati wa mwisho alifurahisha macho yake kwa kumuona yeye mwenyewe na akasema:

كُلُّ مُصِيْبَةٍ بَعْدَكَ جَلَلٌ

“Ewe Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam), kwa baraka ya kukuona, kila dhiki inapungua na kila wasiwasi huondolewa.”

Mapenzi ya maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam)

Mtu fulani aliwahi kumuuliza Ali (radhiyallahu ‘anhu), “Ni mapenzi ya dhaati ya kiasigani maswahaabah walikua nayo kwa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) ?”

Ali (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Mimi na aapa kwa Allah subhaana wata’ala, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa kipenzi zaidi kwetu kuliko mali yetu, watoto wetu na mama zetu, na kuwa karibu nae ilikuwa ni bora zaidi kuliko kinywaji cha maji baridi wakati wa kiu kali.”

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …