Bashara Nzuri Kutoka Kwa Allah( Subhaana Wata’alah) Kwa Wale Ambao Wanamsalia Mtume

عن عبد الرحمن بن عوف رضي الله عنه قال خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم فاتبعته حتى دخل نخلا فسجد فأطال السجود حتى خفت أو خشيت أن يكون الله قد توفاه أو قبضه قال فجئت أنظر فرفع رأسه فقال ما لك يا عبد الرحمن قال فذكرت ذلك له فقال إن جبريل عليه السلام قال لي ألا أبشرك إن الله عز وجل يقول لك من صلى عليك صليت عليه ومن سلم عليك سلمت عليه (مسند أحمد، الرقم: ١٦٦٢، وقال البيهقي في الخلافيات ٣/١٤٣ عن طريق لهذه الرواية بنحو هذه الألفاظ :قال أبو عبد الله – رحمه الله -: هذا حديث صحيح)

Hazrat Abdur Rahmaan Bin Auf (radhiyallahu ‘anhu) alitowa taarifa kuwa kuna wakati mmoja, nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alitoka nyumbani kwake na mimi nikamfuata, mpaka akaingia kwenye shamba la tende na hakashuka chini kusujudu. Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alifanya sajida ndefu mpaka ni kaogopa kuwa mwenyezi mungu tayari amesha mchukuwa. Nilienda mbele yake kuangalia kuna kitu gani kimemkuta nabii wa mwenyezi mungu (sallallahu ‘alaihi wassallam). Kisha nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) aliinuwa kichwa chake cha baraka kutoka sajida na aliniuliza kuna tatizo gani, nikamueleza ni khofu yangu juu yako (yaani kutangulia mbele za haq ukiwa kwenye sajida). Nabii (sallallahu ‘alaihi wassallam) alisema, “(sababu ya kufanya sajida ndefu ilikuwa) jibraeel (alaihis salaam) alikuja kwangu na kusema, ‘si nikupe bashara nzuri allah subhaana wata’alah alivyosema, ‘ yoyote atakae kusalia yaani kumsalia nabii, natuma rehma zangu kwake, na yoyote atakae kutumia salaam, nitatuma utulivu na baraka juu yake huyo mtu.'”

Maswahaba wakijitolea kwa ajili ya Rasulullah (Sallallaahu ‘alaihi wasallam)

Nyumba ya Faatimah (radhiyallahu ‘anha) ilikuwa mbali na nyumba ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) siku moja alimwambia: “Ni matamanio yangu kwamba uishi karibu nami.” Faatimah (radhiyallahu ‘anha) akajibu, “Nyumba ya Haarithah iko karibu na nyumba yako. Ukimwomba abadilishe nyumba yake na yangu, atakubali kwa furaha.” Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, “Tayari amebadilisha mara moja kwa ombi langu. Ninaona aibu kumwomba kwa mara ya pili.”

Basi, Haarithah (radhiyallahu ‘anhu) kwa namna fulani alikuja kujua kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa akitamani Faatimah (radhiyallahu ‘anha) aishi karibu naye. Hapo hapo akamwendea Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) na akasema, “Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam), nimepata kujua kwamba unatamani Faatimah (radhiyallahu ‘anha) aishi karibu nawe. Hizi ndo nyumba zangu. Hakuna nyumba nyingine iliyo karibu na yako zaidi ya hizi nyumba zangu. Faatimah (radhiyallahu ‘anha) anaweza kubadilisha nyumba yake na nyumba yangu yoyote. Ewe Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) unachokikubali kwangu ni kipenzi zaidi kwangu kuliko unachoniachia.”

Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikubali ombi hilo akisema, “Najua kwamba wewe ni mkweli na una ikhlaas katika hayo unayoyasema”, na Rasulullah akamuombea dua.

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …