Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) anapoteza Meno Yake

Wakati wa vita vya Uhud, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alikuwa ameumizwa vibaya sana na adui na vipande viwili vya kofia yake vikapenya kwenye uso wake wa mubarak.

Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu ‘anhu) na Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) mara moja wakakimbia na kumsaidia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Abu Ubaidah (radhiyallahu ‘anhu) akaanza kuong’oa vipande vya kofia kutumia meno yake. Wakati kipande kimoja kilipotolewa, alikuwa amepoteza jino moja. Hakujutia kupoteza kwa jino lake, akatumia tena meno yake kuong’oa kiungo kingine pia.

Alifanikiwa kuong’oa kipande kingine, basi katika harakati hizo, alipoteza jino jingine. Vipande vilipotolewa, damu ilianza kutoka kwenye mwili wa Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) Malik bin Sinaan (radhiyallahu ‘anhu), baba yake na Abu Said Khudri (radhiyallahu ‘anhu), alilamba damu ya Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa mdomo wake. Kwa hili, Rasulullah alisema, “Moto wa Jahannam hauwezi kumgusa mtu ambaye damu yangu imechanganyika na yake.

About admin

Check Also

Hofu Ya Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mali ya Dunia isimfanye Kuto kumcha Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah)

Wakati mmoja, Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipokea dirham laki saba kutoka Hadhramawt. Usiku ule, alipopumzika …