Mahitaji yote ya dunia na ya deeni kutimizw

Habbaan Bin Munqiz (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba sahabi moja aliwahi kumuuliza Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam), "Ewe mjumbe wa Allah (sallallahu alaih wasallam) je nijitolee thuluthi moja ya muda  ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) Alijibu, "ndio, kama utapenda." Ule sahabah akauliza, "je nijitolee thuluthi mbili ya muda ambao nimezitenga kufanya dua ili nitume salaam kwako? "Nabii wa allah akajibu tena, "ndio, kama utapenda. "ule sahabah akauliza, "je nijitolee muda wote kukutumia salaam? "Nabii wa allah (sallallahu alaih wasallam) akajibu, "kama utafanya hivyo, Allah subhaana wata'alah Atayatimiza mahitaji yako yote ambayo unayo (na amboyo ungeulizia kwenye dua yako), ikiwa niyakuhusu dunia au aakhera."

Soma Zaidi »

Mahitaji mia kuitimizwa

Hadrat Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Alisema, "yoyote atakae nitumia salaam mara mia moja kwa kila siku, Allah ta'ala atatimiza mahitaji zake mia, sabini za aakherah na thalathini za duniani."

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 5

27. Kaa kwenye itikafu siku 10 za mwisho za ramadhaani kama unauwezo.

Sayyidina Ibnu Abbaas (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema kuhusu mwenye kukaa itkafu, "mwenye kukaa itkafu (ndani ya msikiti) anajiepusha na madhambi, na kwa wakati wote, anapata thawabu ya kufanya ibada mbali mbali angekuwa na uwezo wa kuzifanya kama asingekuwa kwenye itkafu".

Soma Zaidi »

Thawabu Maalumu Kwa Ajili Ya Kumsalia Nabii Mara Mia Moja

Sayyidina Abuu Hurairah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu alaihi wasallam) amesema "yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara kumi, Allah subhaana wata'alah atatuma salaam kwake mara mia moja, na yoyote atakaye tuma salaam kwangu mara mia moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia salaam kwake mara elfu moja, na yoyote atakaye zidisha (kunisalia mimi) kwa ajili ya upendo (kwa ajili yangu) na kwa hamu (kwa ajili ya kutafuta thawabu), nitamuombea na nitakuwa shahidi kwa ajili yake siku ya mwisho".

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 4

21. Kuna baraka nyingi kwa kuamka muda wa daku. Kwa hiyo mtu atimize sunna ya daku kabla kuanza kufunga.

Sayyidina Abuu Sa'eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema daku inabaraka nyingi. Kwahiyo usiache sunna ya daku, hata kama mtu anaweza kunywa tonye moja la maji muda wa daku (inabidi mtu afanye hivyo ili atimize sunna ya daku.) Kwa hakika Allah subhaana wata'alah ananyunyizia rehema zake maalumu juu ya wale ambao wanaamka muda wa daku na malaika wanawaombea dua maalumu).

Soma Zaidi »

Kupata dua maluum ya wamalaikah

Aamir bin Rabee'ah (radhiyallahu anhu) ameripoti kwamba Nabiii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) alisema, "yoyote atakae niswalia, wamalaikah wataendelea kumswalia yeye (yaani: kumuombea dua) kama ataendelea kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) Kwa hiyo, imebaki kwa mtu kuamua kama atataka kumswalia Nabii wa allah (sallallahu alaihi wasallam) kidogo au kwa wingi."

Soma Zaidi »

Sunna Na Adabu Za Ramadhaani 3

15. Kwenye mwezi wa ramadhaani, jaribu kuzidisha kwa wingi matendo mazuri. Imepokelewa katika hadith kwamba ibada yoyote ile ya nafili (matendo mazuri ya hiyari) yaliyofanyika katika mwezi wa ramadhaani, inamchumia mtu thawabu ya kitendo cha faradhi, na thawabu ya kitendo cha faradhi kilicho fanyika katika mwezi wa ramadhaani kinazidishwa mara sabini

Soma Zaidi »

Thawabu ya yule ambae anamswalia Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) pindi anapo sikia jina tukufu la Nabi wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, "mtu ambae jina langu limetajwa mbele yake anatakiwa atume salamu juu yangu, na kwa hakika yoyote ambae ananitumia salamu mara moja, Allah subhaana wata'alah atamtumia baraka kumi juu yake."

Soma Zaidi »